Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Masanduku ya siri China yaleta taharuki
Kimataifa

Masanduku ya siri China yaleta taharuki

Spread the love

 

SEKTA ya watengeneza wanasesere nchini China imekosolewa kwa kitendo cha kuuza masanduku ya siri ambayo yametumika kusafisisha wanyama. Imeripoti CNN na Mitandao mingine ya habari Duniani … (endelea).

Wakosoaji na watetezi wa haki za wanyama nchi humo wamepinga vikali usafirishwaji wa maboksi hayo baada ya kuonekana yakisafirisha wanyama.

Mdhibiti kutoka kwenye Serikali ya China hivi karibuni alipiga marufuku juu ya uuzaji wa masanduku ya siri kwa watoto chini ya miaka nane na kuweka sharti la idhini ya wazazi kwa watoto wa zaidi ya miaka nane.

Wanaharakati wanapinga uuzaji wa maboksi hayo ya vinyago kwa kueleza kuwa ni ukiukwaji wa haki za watoto na wanyama.

Masanduku hufungwa ka neno siri moja yanawekwa ndani yake midoli ya kuchezea watoto ambapo midoli mingi imekuwa ikienda kinyume cha maadili na kuwapotosha watoto. Pia kwenye maboksi hayo mara kadha kumekutwa wanyama (watoto wa paka au mbwa wakiwa hai).

Uuzaji wa bidhaa hizo mtandaoni uliongezeka zaidi ya asilimia 400 mnamo 2020 ikilinganishwa na 2019.

Kwa mujibu wa Tmall Global Kampuni Pop Mart iliimarija zaidi kwenye biashara hiyo katika 2020 ambapo ilikuwa kampuni pekee iliyochangia zaidi ya asilimia 35 ya mauzo ya nje ya nchi ya masanduku ya siri na mwaka wa 2020 jumla ya mauzo yake yaliongezeka zaidi ya mara 10.

Bidhaa yake maarufu zaidi ilikuwa mwanasesere wa Molly, sanamu ya msichana mdogo iliyoundwa na msanii wa Hong Kong, na sanduku la kuchezea kwa kawaida lilikuwa na bei ya dola za Kimarekani 9.1.

Tovuti za ununuzi nchini Uchina zimeshutumiwa kwa ukatili wa wanyama kwa madai ya kusafirisha masanduku ya siri kwa wateja kukiwa na watoto wa mbwa na paka.

Ripoti za mitaa zilionyesha kuwa wanyama wengi walipata madhara katika usafiri.

CNN ilifichua ukatili wa wanyama nchini China ambapo iligundulika kuwa wanyama walikuwa wakisafirishwa umbali na muda mrefu bila kupewa chakula wala maji.

Kituo cha Uokoaji Wanyama cha Chengdu Love Home kilishiriki kwenye uokoaji wa wanyama mwezi Mei 2021 kikidai kuwa kimepata kreti 160 zenye paka na mbwa nyuma ya lori la kubeba mizigo huko Chengdu.

Video kutoka kwa tukio hilo ilionyesha wanyama waliofadhaika wakiwa wamekusanyika pamoja kwenye masanduku madogo, wakikosa chakula wala maji.

Kituo cha uokoaji kilisema kwamba kiliokoa mamia ya watoto wachanga na paka wakiwa katika hali mbaya wakishindwa kupumua vizuri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaKimataifaTangulizi

Tanzania, Somalia kuibua maeneo mapya ya ushirikiano

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amesema Tanzania na Somalia...

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

error: Content is protected !!