Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya NHIF yafanya uhakiki wanachama, watoa huduma, wafungia vituo 48, waajiri 88
AfyaTangulizi

NHIF yafanya uhakiki wanachama, watoa huduma, wafungia vituo 48, waajiri 88

Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga
Spread the love

 

MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umefanya uhakiki wa wanachama wa mfuko huo na kubaini mambo kadhaa na kuyachukulia hatia ikiwemo kusitisha mikataba yake na vituo vinavyotoa huduma hiyo 48, ikiwa pamoja na kusitisha mikataba ya waajiri 88, sambamba na kuzuia matumizi ya kadi za wanachama 3,589 kutokana na sababu mbalimbali. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamebainika baada ya NHIF kuendesha uhakiki wa wanachana na wanufaika wa mfuko huo uliodumu kwa mwezi mmoja kuanzia Juni mosi, 2023 katika mikoa sita ambayo ni Dar es Salaam, Dodoma, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro na Mwanza.

Uhakiki huo ambao ulikuwa unafanyika kwa njia ya mwanachana kuitwa katika ofisi za mfuko za NHIF pamoja na kuwahakiki katika vituo vya kutolewa huduma ambapo kabla ya mwanachana hajapatiwa huduma anahakikiwa.

Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga amesema katika uhakiki huo uliofanywa kwa mikoa sita wamebaini mambo makubwa matano na kuchukuliwa hatua stahiki na mfuko huo.

Amesema vituo hivyo 48 vimesitishiwa mkataba wake kutokana na kukutwa na udanganyifu katika kutoa huduma wakati wakitoa huduma zao kwa wnaachama wa mfuko huo ambapo waajiri hao 88 wamesitishiwa mikataba yao kutokana ya kugundulika wanachana wanaotokana nao wamekuwa wakikithiri kwa kufanya vitendo vya utanganyifu kwa mara kwa mara.

Konga amesema moja ya mambo waliyobaini ni matumizi mabaya ya kadi za wanachama ambapo kuna baadhi ya kadi za wanachama zimetumiwa na wagonjwa ambao siyo wanachana wa mfuko huo.

Amesema jumla ya kadi 3,589 zimekutwa na mashaka huku ndani yake kadi 1,346 zikiwe zimetumiwa na wagonjwa ambao siyo wanachama wa mfuko wa bima ya afya.

Konga amesema katika uhakiki huo wamebaini pia baadhi ya kadi za wanachama 2290 zimeachwa katika. Vituo vya watoa huduma, hivyo amewataka wanachama wafike katika ofisi za NHIF kwa ajili ya kutambua kazi zao.

Pia wamebaini kuwa baadhi ya wanachama wamekuwa wakitumia nakala ya kadi za uanachama kwa ajili ya kupata huduma, kitendo ambacho ni kinyume na utaratibu hiyo wanatakiwa kufika katika kituoni wakiwa na kadi halisi na siyo nakala yake.

Konga amesema kwa upande wa watoa huduma, wamebaini kuwa baadhi ya hawafuati utaratibu wa kuhakiki wanachama wa mfuko huo hali iliyotoa mwanya kwa wanachama kufanya udanganyifu ukiwemo wa kutumia kadi ambazo siyo za mwanachana sahihi.

Pia Konga amesema pia wamebaini uwepo mtindo wa kumchukulia kadi mgonjwa dawa badala ya mgonjwa kufika mwenyewe hospitali na kumuona daktari na kumuandikia dawa.

“Huu mtindo umechukua kasi, mgonjwa anatoa kadi yake na kumpa mtu mwingine ambaye anaenda hospitali kumchukulia dawa. Napenda kutoa wito kwa wanachama wa bima, wafike wenyewe kwani kumuona daktari na kuandikiwa dawa ni jambo muhimu pia,” alisema Konga.

Konga amesema uhakiki huo ni endelezu ambapoi baada ya kumaliza katika mikoa hiyo sita, awamu inayofuata ni nchi nzima ili kuhakikisha wanachama wanaopatiwa huduma ni wahusika halisi wanaokatwa hela zao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

error: Content is protected !!