March 3, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Marekani yaonyesha uoga kwa Korea Kaskazini

Spread the love

MAREKANI imeapa kujibu shambulio lolote la kijeshi kutoka Korea Kaskazini dhidi ya nchi hiyo ama washirika wake, anaandika Irene David.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Ulinzi wa Marekani, James Mattis, wakati akizungumza na Rais Donald Trump, katika mkutano wa kuzungumzia masuala ya ulinzi katika taifa hilo kufuatia jaribio la bomu la Nyuklia huko Pyongyang lililofanywa na Korea Kaskazini.

Trump ameonya kuwa Marekani inaweza kusimamisha kufanya biashara na nchi yoyote inayoshirikiana kibiashara na Korea Kaskazini.

Amesema kuwa haamini kama Korea Kaskazini inaweza kuishambulia Marekani na itafanya jitihada zozote ili kuweza kuondoa mzozo huo.

error: Content is protected !!