March 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Kamera ya kupiga picha ndani ya mwili wa binadamu yagunduliwa

Kifaa cha Endoscope chenye uwezo kupiga picha ndani ya mwili wa binadamu

Spread the love

WANASAYANSI nchini Uingereza wamegundua kamera yenye uwezo ya kupiga picha viungo vya ndani ya mwili wa binadamu, anaandika Mwandishi Wetu.

Kifaa hicho kimeundwa kuwasaidia madaktari kusaka vifaa vya madaktari, vinavyofahamika kama endoscopes, ambavyo huenda vinaweza kubakia ndani ya viungo vya binadamu wakati wa upasuaji.

Hadi sasa, matabibu wamekuwa wakitegemea uchunguzi unaogharimu fedha nyingi, kama vile picha za X-ray, ili kufuatilia mafanikio yao.

Kamera hiyo mpya, itafanya kazi ya kubaini mwanzo wa mwangaza ndani ya mwili wa binadamu, kama vile sehemu ya ncha ya mwisho ya kifaa cha upasuaji cha tube ya endoscope.

Kifaa hicho kimeundwa kuwasaidia madaktari kusaka vifaa vya kimatibabu vinavyojulikana kama endoscopes mwilini mwa binadamu

Profesa Kev Dhaliwal, wa Chuo Kikuu cha Edinburgh, anasema: “Ina uwezo mkubwa wa kutumika katika hali tofauti tofauti, kama vile inavyoelezwa ikiwa kazini.

“Uwezo wa kuona kilipo kifaa kilichosahaulika ndani ya mwili wa binadamu hasa katika sekta mbalimbali katika sekta ya afya, huku tukisonga mbele kupunguza hali na mbinu ya kila aina ya kutibu maradhi mbalimbali.”

Majaribio ya awali, yanaonyesha kifaa cha Prototype, kinaweza kubaini na kufuatilia mwangaza kupitia eneo la mshipa wa sentimita 20, katika hali tu ya kawaida.

Miali ya mwangaza kutoka Endoscope, inaweza kupenyeza ndani ya mwili, lakini mara nyingi hutawanyika au kuangazia nje ya mshipa na viungo, badala ya kupenyeza moja kwa moja mwilini.

error: Content is protected !!