August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Marekani kushambuliwa na makombora

Mifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini

Spread the love

NCHI ya Korea Kaskazini inapanga kurusha makombora karibu na kisiwa kimoja nchini Marekani Korea imesema kwamba inatafakari uwezekano wa kurusha makombora karibu na jimbo la Marekani la Guam katika bahari ya Pasifiki, anaandika Hellen Sisya.

Kauli ya nchi hiyo inakuja muda mchache baada ya Rais Donald Trump wa Marekani kuitishia Pyongyang kwamba itakabaliwa na “ghadhabu.”

Shirika la habari la Korea Kaskazini limesema taifa hilo linatafakari mpango wa kurusha makombora ya masafa ya kati ya umbali karibu na Guam, eneo ambalo Marekani huwa na ndege zake za kuangusha mabomu.

Taarifa hiyo inaashiria kuongezeka kwa uhasama kati ya nchi hizo mbili na kivi karibuni Umoja wa Mataifa UN, uliidhinisha vikwazo zaidi vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo.

error: Content is protected !!