August 17, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwenyekiti wa Tume Kenya amtuliza Raila Odinga

Wafula Chebukata, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka ya Kenya (IEBC)

Spread the love

WAFULA Chebukati, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi na Mipaka Nchini Kenya (IBEC), ameahidi kushughulikia malalamiko yaliyotolewa na mgombea urais kupitia Muungano wa NASA, Raila Odinga, juu ya kuwepo kwa madai ya udanganyifu kwenye uhesabuji wa kura, anaandika Victoria Chance.

Amesema fomu 34A na 34B ziko tayari na wameandaa dawati la mawakala wakuu kwaajili ya kuchunguza fomu 34A na 34B, “…tutajua kama haya malalamiko ni ya kweli na kama siyo ya ukweli hatutayazingatia.”

Chebukati amewataka Wakenya kuvuta subira na matokeo ya mwisho bado hayajatolewa na kwamba yatatolewa baada ya siku tano kuanzia leo.

Leo mapema asubuhi, Odinga aliitaka Tume hiyo kuhakikisha inatumia fomu namba 34 A kama sheria inavyotaka, wakati wa kujumlisha na kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu nchini Kenya.

error: Content is protected !!