Wednesday , 24 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Matenki ya mafuta kujengwa Tanga
Habari Mchanganyiko

Matenki ya mafuta kujengwa Tanga

Matanki ya GBP yaliyopo mkoani Tanga
Spread the love

KAMPUNI ya mafuta ya GBP imepanga kutumia zaidi ya 60 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa bohari ya kuhifadhia mafuta na kiwanda cha gesi ili kuongeza huduma na kupunguza kero ya upatikanaji wa bidhaa hizo, anaandika Mwandishi Wetu.

Mkurugenzi wa GBP, Badar Sood alieleza kuwa kampuni hiyo ina mpango wa kujenga matenki zaidi yenye uwezo wa kuhifadhi lita 300 na kwamba bohari ya sasa inahifadhi lita million 122.6.

Sood amesema sambamba na ujenzi wa matanki hayo ambayo mradi wake umezinduliwa juzi na Rais John Magufuli, utaambatana na mpango wa kujengwa kwa kiwanda cha gesi ambavyo vyote kwa pamoja vinatarajiwa kugharimu jumla ya Sh. 60 bilioni.

“Ujenzi wa matenki hayo umepunguza foleni ya malori jijini Dar es Salaam pamoja na uharibifu wa barabara” ameeleza Sood.

Ameeleza ya kampuni hiyo kuwa pamoja na mambo mengine ni kufanya uwekezaji mkubwa kwa kutumia meli kubwa na hivyo kupunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa hiyo.

Katika kusaidia jamii, Mkurugenzi huyo ameleza kuwa uwekezaji wake umejikita katika ushiriki wa harakati za maendeleo ikiwemo kuchangia sekta ya elimu kwa kutoa jumla ya mifuko 2000 ya saruji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

THRDC yaongeza mkataba wa ushirikiano na ABA

Spread the love  MTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC),...

Habari Mchanganyiko

Rufaa ya Equity Benki, State Oil yakwama

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imeshindwa kuendelea na...

Habari Mchanganyiko

Bodaboda waeleza mafanikio mafunzo usalama barabarani

Spread the loveMADEREVA bodaboda katika Jiji la Dodoma wameeleza jinsi mafunzo ya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yaahidi kuendelea kuunga mkono Serikali za Mitaa

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesisitiza dhamira yake ya...

error: Content is protected !!