July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mapendekezo mapya tozo za simu yamfikia Majaliwa

Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania

Spread the love

 

HATIMA ya kufutwa au kupunguzwa kwa tozo ya miaka ya mitandao ya simu itajulikana wakati wowote kuanzia sasa, baada ya kamati iliyoundwa kupitia maoni ya wananchi juu tuzo hiyo kukamilisha kazi yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea). 

Kamati hiyo iliyokuwa ikiundwa na wataalamu mbalimbali wakiwemo mawaziri waziri wa fedha na mipango, Dk. Mwigulu Nchemba na wa mawasiliano na teknolojia, Dk. Faustine Ndugulile, kumkabidhi taarifa hiyo.

Jana Jumamosi, tarehe 31 Julai 2021, mawaziri hao, walimkabidhi taarifa hiyo Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Tozo hizo zinazolalamikiwa na wananchi, zilianza kutumika kuanzia tarehe 15 Julai 2021 na kumfanya Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kuagiza kupitia malalamiko hayo ya wananchi na kuyafanyia kazi.

Dk. Faustin Ndungulile

Leo Jumapili, tarehe 1 Agosti 2021, Msemaji Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Gerson Msigwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam amesema, Dk. Mwigulu na Dk. Ndugulile jana Jumamosi, waliwasilisha taarifa yao kwa Waziri Mkuu, Majaliwa.

“Wamewasilisha mapendekezo ya namna ya kufanyiakazi na waziri mkuu ametoa maelekezo mengine ya kwenda kuiweka sawa na wakati wowote serikali itakuja na maelezo,” amesema Msigwa ambaye pia ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo.

“Hii tozo imewekwa na sheria na ukitaka kuiondoa lazima urudi bungeni lakini kuna kipengele cha kanuni ambacho waziri anaaandaa namna ya utozaji na taarifa ya kwanza imetolewa jana, sasa tusubiri baada ya hapo itasemaje na Watanzania wataelezwa namna tunakwenda,” amesema.

Dk. Mwigulu Nchemba, Waziri wa Fedha na Mipango

Msigwa amesema, lengo la Serikali ni kuhakikisha inaongeza nguvu katika kukabiliana na matatizo ya hali mbaya za barabara hasa vijijini, kujenga vituo vya afya, hospitali, zahanati, kupeleka maji na huduma nyingine za kijamii.”

“Hili la tozo liliwekwa kwa lengo zuri na Mheshimiwa Mwigulu anaiita tozo ya mshikamano na ukiwa Dar es Salaam huwezi kujua maumivu wanayopata kule kijijini ya kukosa barabarani, huduma bora za afya na elimu ambapo hii tozo ndiyo inakwenmda kutatua haya matatizo na kule kijijini wanasubiri sana hizi fedha,” amesema Msigwa

Tarehe 27 Julai 2021, Ikulu jijini Dar es Salaam, Rais Samia akiwaapisha mabalozi 13 aliowateua 22 Mei 2021, alizungumzua suala hilo la tozo kwenye hotuba yake akisema, Serikali haitaiondoa tozo hiyo, bali itaangalia njia nzuri ya kuitumia pasina kuathiri wananchi.

“Hizi tozo nataka niseme zipo, ila tutaangalia njia nzuri ambayo haitaumiza watu. Serikali ipate na wananchi wapate kazi iendelee,” alisema Rais Samia.

Alisema, Serikali yake iliamua kuweka tozo hiyo ili ipate fedha za kutekeleza miradi ya maendeleo, itakayosaidia kutatua changamoto za wananchi ikiwemo, uhaba wa maji na ubovu wa miundombinu ya barabara.

error: Content is protected !!