July 1, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia awapongeza vijana U23, atoa maagizo

Spread the love

 

SAMIA Suluhu Hassan, Rais wa Tanzania ameipongeza timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 23 (U23), kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA-2021). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Timu hiyo ilitwaa ubingwa huo tarehe 30 Julai 2021, nchini Ethiopia kulikofanyika michuano hiyo kwa kuwafunga kwa penati vijana wenzao kutoka Burundi kwa 6-5.

Ni baada ya dakika 90 kumalizika kwa kutokufungana.

Leo Jumapili, tarehe 1 Agosti 2021, timu hiyo imerejea nchini na kupokelewa na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallece Karia, ameipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam.

Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia ukara wake wa kijamii wa twitter akisema “Nawapongeza timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 23 kwa kutwaa ubingwa wa Mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA-2021).”

“Ushindi huu ni heshima kwa nchi yetu na ni chachu ya kukuza michezo. Natoa wito kwa wadau wa michezo kuendeleza jitihada za kukuza michezo yetu,” amesema

error: Content is protected !!