February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Makombora ya Korea Kaskazini yaitikisa Japan

Mifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini

Spread the love

KOREA Kaskazini imerusha makombora kuelekea mashariki mwa kisiwa cha Hokkaido kwa umbali wa kilomita 1000, anaandika Irene David.

Waziri Mkuu wa Japani Shinzo Abe, amesema urushwaji huo wa makombora haujawahi kutokea na umeleta hofu kubwa kwa taifa lake.

Tishio hilo limesababisha watu nchini humo kujificha maeneo yaliyo chini ya ardhi ama kwenye majengo yaliyoimara kama moja ya kutafuta usalama wao.

Wanajeshi wa Marekani na wale wa Japani wanafanya mazoezi katika eneo hilo la Hokkaida, Abe na Rais wa Marekeani, Donald Trump, wameungana na kukubaliana kuiongezea shinikizo Korea Kaskazini.

Tukio hilo limekuwa tishio kwa Japani kwani Korea Kaskazini haijawahi kurusha Makombora ya juu ya ardhi nchini humo.

error: Content is protected !!