March 7, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mawakili wamtosa Lissu Dar

Spread the love

SAKATA la Mawakili binafsi kutakiwa kugoma kufanya kazi leo limetibuka baada ya kubainika baada ya baadhi yao wamekaidi agizo la Rais wa Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS), Tundu Lissu la kuwataka wanasheria hao kugoma, anaandika Mwandishi wetu.

Mwishoni mwa  wiki Lissu aliwataka Mawakili kugoma kufanya kazi zao kama namna ya kupinga tukio la ulipuliwaji wa Ofisi ya Mawakili wa IMMMA ya jijini Dar es Salaam.

Hata hivyo, MwanaHALISI Online leo imeshuhudia Mawakili hao wakiendelea na kazi zao kama kawaida katika mahakama mbalimbali jijini Dar es Salaam.

Wakili Alibart Msando amesema ameshindwa kugoma kwa kuwa leo tayari alikuwa amechukua kazi za watu ambao wamemlipa fedha.

” Kuna kesi ambazo huwezi kuziepuka kuna watu wana kesi  muhimu na wengine wana mali zao wanataka ziuzwe na kama nisingetokea kesi ingeweza kufutwa,” amesema

error: Content is protected !!