Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Maisha Burudika Makali ya Skillager kwenye ‘Busy Body’ usipime!
Burudika

Makali ya Skillager kwenye ‘Busy Body’ usipime!

Spread the love

MWANAMUZIKI anayekuja kwa kasi kwenye game ya Afro Pop, Felix Philemon Sola ‘Skillager’ ameachia kitu kipya, ‘Body Busy’. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Msanii huyo ambaye licha ya kuimba ni mtumbuizaji na mwandishi wa mashairi, ameachia jiwe hilo moto, akiwa chini ya Lebo ya Tree of Life Entertainment ya nchini Nigeria.

 Wimbo huu wa kusisimua ni heshima kwa wanawake wa Kiafrika, ukiakisi kusherehekea nguvu, urembo na ujasiri wa mwanamke wa Kiafrika.

 ‘Busy Body’ unazungumzia shamrashamra za wanawake wa Kiafrika, ambao mara nyingi ndio nguzo ya familia na jamii zao.

 Utundu wa kipekee wa Skillager na mtazamo mpya unamfanya kuwa kinara katika ulimwengu wa muziki wa Afro Beat.

 Muziki wake unazungumzia juu ya mapambano na ushindi wa watu wa kila siku, huku ukisisitiza watu kutokuwa wabaguzi.

Tayari kibao hicho, ‘Busy Body’ kinapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii inayodili na muziki, hivyo basi tembelea sasa ili kutoa sapoti kwa staa huyu ajaye, lakini pia kupata ladha ya aina yake kwa mwanamuziki huyu anayekuja kwa kasi ya kimbunga.

 Msanii huyu ni mzaliwa wa Jimbo la Adamawa, akiwa amekulia Ebonyi, kusini kwa Nigeria.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BurudikaMichezo

Kizz Daniel aunguruma na EP mpya ‘Thankz alot’

Spread the loveMKALI wa muziki nchini Nigeria, Kizz Daniel ametoa EP yake...

BurudikaHabari za Siasa

Samia amchangia Professa Jay mil. 50, Chadema, wasanii wamwaga manoti

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amechangia kiasi cha Sh 50 milioni...

Burudika

Piga makofi kwa Mr. Eazi …achomoka na ‘The Evil Genius’

Spread the loveMAKOFI kwa Mr Eazi! Staa wa Afropop, Mr Eazi ameachia...

Burudika

Kishindo cha Afro B katika “Wo wo wo” akiwa na Rich the Kid&Rimzee

Spread the loveSTAA ambaye alitambulishwa na ngoma maarufu, Afrowave ‘Drogba’, Afro B,...

error: Content is protected !!