Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kesi kina Mdee:Dk. Lwaitama asema atatetea uanachama wao wakiachia ubunge
Habari za Siasa

Kesi kina Mdee:Dk. Lwaitama asema atatetea uanachama wao wakiachia ubunge

Spread the love

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Prof. Azavel Lwaitama, amesema atakuwa wa kwanza kuwatetea wabunge viti maalum 19, warejeshewe uanachama wao, endapo watakubali kutoka bungeni. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar ea Salaam … (endelea).

Akihojiwa maswali ya dodoso katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam na Wakili wa wabunge hao, Ipilinga Panya, leo tarehe 10 Machi 2023, Prof. Lwaitama amedai kosa la wabunge hao ni kuingia bungeni jijini Dodoma kinyume cha sheria.

Mbele ya Jaji Cyprian Mkeha, Prof. Lwaitama alidai ” hata leo hii wakitoka bungeni nitakuwa wa kwanza kuwatetea warudi kwenye chama.”

Baada ya kutoa kauli hiyo, Wakili Panya alimhoji iwapo shida ni bungeni ambapo Prof. Lwaitama alijibu akidai “utaratibu ni batili, wa kihuni wa kuingia bungeni. Mtu kaachiwa, katolewa gerezani usiku, ku- forge barua, hiyo ndiyo haitakiwi. Tunajenga taifa la namna gani? Hoja sio wao ni utaratibu.”

Prof. Lwaitama anahojiwa maswali hayo kuhusu hati zao za kiapo kinzani walizowasilisha mahakamani hapo kujibu Kesi Na. 36/2022, iliyofunguliwa na wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee.

Mdee na wenzake 18, wamefungua kesi hiyo wakipinga uamuzi wa Chadema kuwafukuza uanachama kwa madai kuwa haukuwa halali, ambapo wanaiomba mahakama ifanye mapitio dhidi ya mchakato uliotumika kuwafukuza Chadema.

Prof. Lwaitama anaendelea kuhojiwa maswali mahakamani hapo.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online kwa taarifa zaidi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

ACT: Waongoza watalii wapate maslahi yao inavyostahili

Spread the loveCHAMA cha ACT-Wazalendo kimeitaka serikali kuhakikisha inasimamia maslahi stahiki ya...

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

error: Content is protected !!