Friday , 19 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Majaji wanawake waongezeka, Jaji Mkuu awapa changamoto
Habari Mchanganyiko

Majaji wanawake waongezeka, Jaji Mkuu awapa changamoto

Spread the love

 

JAJI Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma, amewataka majaji na mahakimu wanawake nchini, kuwa mstari wa mbele katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), ili wasiachwe nyuma. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam …(endelea).

Prof. Juma ametoa wito huo leo tarehe 10 Machi 2023, katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya majaji na mahakimu wanawake duniani, yaliyoandaliwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Wanawake Tanzania (TAWJA) na kufanyika jijini Dar es Salaam.

“Kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya mwanamke duniani inachochea matumizi ya kidigitali kwa wote, ugunduzi wa teknolojia na matumizi ya kidigitali, huu usawa tunaouzungumzia tusipoweza kuziba pengo katika eneo la teknolojia tutazidi kuachwa nyuma,” amesema Prof. Juma.

Prof. Juma amesema matumizi ya TEHAMA yanarahisha utekelezaji wa shughuli mbalimbali.

Kiongozi huyo wa mahakama, amewataka majaji na mahakimu wanawake kuendelea kujipanga ili waweze kulinda na kutenda haki katika utekelezaji wa majukumu yao.

Amewataka kuandika vitabu vinavyoelezea changamoto na mafanikio wanayokutana nayo katika utekelezaji wa majukumu yao, ili kuwashawishi wanawake wengi zaidi kuingia katika kazi yao.

Prof. Juma amesema ongezeko la majaji, mahakimu na watendaji wa mahakama wanawake, limeongeza ufanisi wa utekelezaji majukumu ya mahakama, kwa kuwa wana uwezo mkubwa katika uongozi.

“Uwepo wa majaji wanawake unaongeza utoaji haki kwa jamii, sababu uwepo wao unaongeza imani ya wananchi kwa mahakama. Lakini unahamasisha vizazi vijavyo vya wasichana ambao atamuona jaji kama mfano wa kufikia nafasi hiyo,” amesema Prof. Juma.

Awali, Mwenyekiti wa TWJA, Jaji Sehel Barke, alisema idadi ya majaji na mahakimu wanawake nchini imeongezeka kwa asilimia 30.

Jaji Barke amesema takwimu za Desemba 2022, zinaonyesha majaji wanawake ngazi ya rufaa imeongezeka kwa asilimia 38, ambapo wanawake ni 10 wakati wanaume wakiwa 16.

Amesema idadi ya wanawake ngazi ya mahakama kuu imeongezeka kwa asilimia 36 na kwamba wanawake ni 35 na wanaume 36.

Kwa upande wa ngazi ya mahakama za wilaya, amesema idadi ya wanawake imeongezeka kwa asilimia 50, ambapo wanawake ni 141 na wanaume 141.

Jaji Barke amesema maadhimisho hayo yatumika kujadili mafanikio na changamoto zinazowakabili majaji na mahakimu wanawake ili kuja na maadhimio ya kuboresha utendaji wao.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

Habari Mchanganyiko

Carbon First, Ruangwa wasaini makubaliano ya biashara ya hewa ukaa

Spread the love  KAMPUNI ya Carbon First Tanzania Limited na Halmashauri ya...

Habari Mchanganyiko

CBE yawakumbuka wenye mahitaji maalum Jangwani

Spread the loveCHUO cha Elimu ya Biashara (CBE), kimetoa msaada mbalimbali na...

Habari Mchanganyiko

Mume auwa mke kwa kumchoma visu, ajisalimisha Polisi

Spread the loveJACKSON Kalamji (49), anashikiliwa na Jeshi la Polisi jijini Mwanza,...

error: Content is protected !!