Wednesday , 29 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Lwaitama aeileza mahakama kina Mdee walivyomtesa Mbowe
Habari za Siasa

Dk. Lwaitama aeileza mahakama kina Mdee walivyomtesa Mbowe

Freeman Mbowe, Mwenyekiti Chadema Taifa
Spread the love

 

MJUMBE wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Azavel Lwaitama, amedai wanachama 19 waliofukuzwa na chama hicho walimtesa Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe, kufuatia uamuzi wao wa kuukubali ubunge viti maalum kinyume cha sheria. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Dk. Lwaitama ametoa madai hayo leo tarehe 10 Machi 2023, akihojiwa maswali ya dodoso na Wakili wa wabunge hao wa viti maalum, Ipilinga Panya, katika Mahakama Kuu, Masjala Kuu, jijini Dar es Salaam, mbele ya Jaji Cyprian Mkeha.

Alitoa madai hayo baada ya video yenye hotuba ya Mbowe akimtaka kiongozi wa wabunge hao, Halima Mdee, kuomba radhi kwa hatua waliyofanya mbele ya wajumbe wa Baraza Kuu la Chadema.

Kufuatia hotuba hiyo, Wakili Panya, alimhoji ni utaratibu wa kawaida wa Chadema kurekodi video katika mikutano yake wakati inaendelea.

Ambapo Dk. Lwaitama alijibu “sababu siku hizi watu wanarusha moja kwa moja mitandaoni kusikiliza hotuba, baadae sijui kama ilirekodiwa kwa ajili ya kuletwa mahakamani.”

“…inaeleza mateso aliyopata Mbowe kuomba warudi kwenye kundi na kuwaomba watubu kurudi kwenye kundi, turudi kwenye kazi,” amedai Dk. Lwaitama.

Alidai Mbowe alimuomba Mdee kuomba radhi kwa kuwa alikuwa na uwezo wa kuwashawishi wenzake waombe radhi.

Dk. Lwaitama amedai kuwa, Mbowe alikuwa anajaribu kuwashawishi waombe radhi ili asiwapoteze lakini ilishindikana.

Kikao hicho cha Baraza Kuu la Chadema, kilifanyika Mei 2022, ambapo kilitupilia mbali rufaa ya wabunge hao kupinga kuvuliwa uanachama.

Kesi hiyo inaendelea kusikilizwa mahakamani halo mbele ya Jaji Mkeha, ambapo Dk. Lwaitama anaendelea kuulizwa maswali ya dodoso na Wakili Panya, kuhusu hati kiapo kinzani walichowasilisha mahakamani kujibu malalamiko ya kina Mdee.

Mdee na wenzake wamefungua kesi hiyo Na. 36/2022 mahakamani hapo, kupinga kufukuzwa Chadema bila kupewa nafasi ya kusikilizwa.

Endelea kufuatilia MwanaHALISI Online.

2 Comments

  • Mh mwekiti hao wabunge 19 yaani Halima mdee na wenzake ni wasaliti na walipewa nafasi ya kuomba radhi wakakaidi kwa maslahi yao binafsi naomba wasitambulike na chama waendelee kutambulika na Ndugai basi inatosha. Mwisho wa ubaya ni aibu

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

TEMESA iliyokarabati Kivuko kwa Bil 7.5 yapata hati chafu

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

ACT-Wazalendo yakusanya Mil 8.5/- kodi ya zuio na kutokomea nazo

Spread the love  MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG),...

Habari za Siasa

DC Kasilda Mgeni ahamasisha chakula shuleni

Spread the love  MKUU wa Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, Kasilda Mgeni...

Habari za Siasa

Bilioni 223.9 zapelekwa Tunduru ndani ya miaka 2 ya SSH

Spread the love  ZAIDI ya Sh. bilioni 223.9 zimepelekwa Wilaya ya Tunduru...

error: Content is protected !!