Wednesday , 6 December 2023
Home Kitengo Maisha Afya Majengo ya mil. 500 kuanza kutoa huduma za afya mwezi huu Manyoni
Afya

Majengo ya mil. 500 kuanza kutoa huduma za afya mwezi huu Manyoni

Spread the love

Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Festo Dugange amesema katika mwaka wa fedha 2023 Serikali imetoa kiasi cha Sh. 500 milioni kwa ajili ya ujenzi wa wodi mbili za wanawake na wanaume pamoja na jengo la kuhifadhia maiti katika hospitaali ya Wilaya ya Manyoni. Anaripoti Jemimah Samwel …(endelea).

Amesema majengo hayo yamekamilika na yataanza kutumika mwisho wa mwezi huu wa Novemba.

Dugange ametoa kauli hiyo bungeni jijini Dodoma leo tarehe 8 Novemba 2023 wakati alijibu swali la Mbunge wa Viti Maalumu CCM, Aysharose Mattembe aliyehoji Serikali ina mpango gani wa kukarabati hospitali ya wilaya ya Manyoni  mkoani Singida ili kusaidia wakazi wa Wilaya hiyo kupata huduma za afya kwa urahisi.

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo amesema katika mwaka wa fedha 2023 serikali imepeleka Sh 1.4 bilioni Oktoba 2023 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa hospitali ya wilaya hiyo.

“Halmashauri inaendelea na utaratibu wa kupata mzabuni kwa ajili ya ujenzi wa wodi ya wazazi,jengo la dharura,stoo ya kuifadhia dawa,jengo la kliniki ya mama na mtoto,jengo la kufulia pamoja na majengo mengine ya hospitali,” amesema Dugange.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

AfyaHabari Mchanganyiko

Majaliwa aipongeza GGML mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveWaziri Mkuu Kassim Majaliwa ameipongeza Kampuni ya Geita Gold Mining...

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

AfyaMichezo

GGML yatoa milioni 17 kung’arisha ATF Marathon

Spread the loveKATIKA kuendelea kuunga mkono jitihada za Serikali kukabiliana na maambukizi...

error: Content is protected !!