Wednesday , 6 December 2023
Home Kitengo Michezo Klabu za Tz Bara zakaribishwa kutumia viwanja Zanzibar
Michezo

Klabu za Tz Bara zakaribishwa kutumia viwanja Zanzibar

Spread the love

NAIBU Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo  Hamis Mwinjuma  maarufu kama MwanaFA amesema timu yoyote inayoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara inakaribishwa kuchagua uwanja wa Amani au Gombani Visiwani Zanzibar kuwa uwanja wake wa nyumbani kwa kuwa hakuna kikwazo chochote. Anaripoti Jemimah Samwel …(endelea).

Amesema Ligi Kuu ya NBC inaendeshwa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na utekelezaji wake unasimamiwa na Bodi ya Ligi Tanzania

Mwinjuma ametoa kauli hiyo bunge ni jijini Dodoma leo terehe 8 Novemba 2023 wakati akijibu swali la mbumge wa Gando Mussa Omar aliyehoji ni kwa nini Ligi kuu ya Tanzania baadhi ya mechi zisichezwe kwenye viwanja vya Gombani na Amani vilivyopo Pemba na Unguja?

Akijibu swali hilo Naibu Waziri huyo kabla ya Ligi kuanza timu zina uhuru wa kuchagua uwanja wake wa nyumbani ambao utatumika kwa michezo yake yote ya nyumbani.

“Timu yeyote itawiwa kuchagua uwanja wa Amani au Gombani kuwa uwanja wake wa nyumbani hakutakuwa na kikwazo chochote endapo watakidhi makubaliano na uongozi unaosimamia taratibu na matumizi ya uwanja husika bila kuathiri Kanuni na Miongozo ya Kamati za Ligi za TFF na ZFF.

Aidha, amesema kanuni ya 9:7 ya Bodi ya Ligi inaruhusu timu ya Ligi Kuu kuteua viwanja vingine miongoni mwa viwanja visivyokuwa na michezo ya Ligi Kuu kwa michezo yake miwili tu a nyumbani na kuwasilisha uteuzi wake siku 21 kabla ya mchezo husika inayokusudia kucheza kwenye uwanja ulioteuliwa.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Piga mkwanja wa kutosha katika usiku wa kibabe kati ya Man United vs Chelsea

Spread the love USIKU wa leo katika dimba la Old Trafford utapigwa mchezowa...

BiasharaMichezo

Mwana FA anogesha Tamasha la Exim Bima Festival

Spread the loveNAIBU Waziri Wa Utamaduni, Sanaa Na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana...

Michezo

Manchester City dhidi ya Tottenham ni usiku wa kisasi

Spread the love KIPUTE kati ya klabu ya Manchester City dhidi yaTottenham Hotspurs...

Michezo

Wikiendi ya kutamba na Meridianbet hii hapa usikubali kuikosa

Spread the loveMERIDIANBET wanakwenda kukupa nafasi ya kutambawikiendi hii kupitia ODDS KUBWA walizoweka...

error: Content is protected !!