Thursday , 7 December 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Mahakama: Sabaya hakufanya ujambazi
Habari za SiasaTangulizi

Mahakama: Sabaya hakufanya ujambazi

Spread the love

ALIYEKUWA Mkuu wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya ameibwaga tena Serikali mahakamani katika kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha, baada ya Mahakama ya Rufani jijini Arusha, kutoa uamuzi kwamba hakufanya tukio la ujambazi, bali alikuwa anatekeleza majukumu yake. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha…(endelea).

Uamuzi huo umetolewa leo tarehe 17 Novemba 2023, jijini Arusha na jopo la majaji watatu, likiongozwa na Jaji Jacob Mwambegele.

Ni katika rufaa iliyokatwa na ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), kupinga uamuzi uliotolewa Aprili 2023 na Mahakama Kuu, mbele ya Jaji Sedekia Kisanga wa kutengua hukumu iliyotolewa na Hakimu Odira Amoro, wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ya kifungo cha miaka 30 jela.

Baada ya mahakama hiyo kumwacha huru Sabaya,ofisi ya DPP alifungua rufaa hiyo ikidai kuwa imethibitisha pasina shaka kuwa Sabaya na wenzake wawili, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura, kuwa walifanya tukio la unyang’anyi wa kutumia silaha, mnamo tarehe 2 Februari 2021, maeneo ya Soko Kuu la Arusha.

Licha ya ofisi DPP kutoa hoja hiyo, jopo la majaji watatu, leo limetoa uamuzi wa kwamba, hakujawahi tokea tukio la ujambazi, badala yake Sabaya alikuwa anatekeleza majukumu yake halali kama kiongozi wa umma, kufuatilia makosa ya uhujumu uchumi kama ilivyoelezwa na mashahidi wa jamhuri.

Lengai Ole Sabaya 

Akizungumza baada ya mahakama kutoa uamuzi uliompa ushindi, Sabaya alimshukuru Mungu akisema “Mungu awabariki sana, aliyefanya ni Mungu mwenyewe. Haki imeshinda.”

Hii ni mara ya pili kwa mahakama kutoa uamuzi uliompa ushindi Sabaya na wenzake, ambapo mara ya kwanza ilitokea katika mahakama kuu, ambayo ilitengua adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela, baada ya kumkuta Sabaya na wenzake kuwa hawana hatia katika mashtaka ya unyang’anyi wa kutumia silaha.

Awali, Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, ilitoa adhabu hiyo baada ya kumkuta na hatia Sabaya na wenzake.

Katika kesi hiyo, Sabaya na wenzake walikuwa wanakabiliwa na mashtaka ya unyang’anyi, wakidaiwa kuchukua kwa nguvu fedha kiasi cha Sh. 399,000 kutoka kwa Diwani wa Sombetini, Bakari Msangi. Sh. 2 milioni za mfanyabiashara na Sh. 39,000 za Ramadhan Ayub pamoja na simu yake ndogo aina ya Tekno.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Bashungwa: Katesh kutafanyiwa usafi wa hali ya juu

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa amesema kazi ya kuondoa tope...

AfyaHabari za Siasa

RAS Songwe: Tumepigwa… mkurugenzi nakupa siku 21

Spread the loveKATIBU tawala mkoani Songwe, Happines Seneda ametoa siku 21 kwa...

BiasharaTangulizi

Bei ya Dizeli, Petroli yashuka

Spread the loveBEI ya mafuta kwa mwezi Disemba, imeshuka kutokana na kupungua...

Habari za Siasa

Dk. Biteko: Viongozi tuache alama nzuri katika utendaji wetu

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

error: Content is protected !!