Thursday , 7 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Polisi Dar wazima tukio la ujambazi Kigamboni
Habari Mchanganyiko

Polisi Dar wazima tukio la ujambazi Kigamboni

Spread the love

JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuzima tukio la ujambazi uliopangwa kufanyika katika eneo la Kampuni ya Kijiji Park, iliyoko Kibada Kigamboni, wilayani Temeke, Mkoa wa Dar es Salaam.Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 17 Novemba 2023, Kamanda wa kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro, amedai kundi la watu sita wanaodaiwa kuwa majambazi wakiwa na silaha za jadi, walivamia eneo hilo usiku wa jana Alhamisi, kwa lengo la kutaka kuiba mafuta yaliyohifadhiwa chini ya ardhi.

Kamanda Muliro amedai kuwa, kundi hilo baada ya kuingia ndani ya eneo wakiwa na gari aina ya fuso walianza  kumfunga kamba mlinzi kisha kuanza kuiba mafuta. Lakini kabla hawajamaliza polisi walifika na kuanza kuwadhibiti.

“Jeshi la Polisi baadae lilipata taarifa toka kwa watu wema na kufika haraka eneo la tukio.Alikutwa mlinzi akiwa kwenye hali mbaya akaokolewa na baadae wahalifu hao walijaribu kuwashambulia askari ambao walijihami haraka na kuwajeruhi wawili miongoni mwao kwa risasi,” amesema Kamanda Muliro na kuongeza:

“Watuhumiwa hao walipelekwa hospitali wakiwa na hali mbaya na majina yao hayajafahamika. Mtuhumiwa mwingine  aliyekamatwa eneo la tukio ni Nelson Mbewe (49), mkazi wa Ubungo Kibangu na anahojiwa kwa kina juu ya tuhuma hizo za unyang’anyi wa kutumia silaha kwa kuvamia eneo hilo. Wahalifu wengine wanaendelea kusakwa na lazima watakamatwa.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Shura ya Maimamu kukata rufaa kupinga Sheikh kufungwa miaka 7

Spread the loveSHURA ya Maimamu Tanzania, inakusudia kukata rufaa dhidi ya hukumu...

Habari Mchanganyiko

TMA yaagizwa kutangaza mafanikio yao kikanda, kimataifa

Spread the love  KATIBU Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara ameiagiza...

Habari Mchanganyiko

NMB yasaidia waathirika wa mafuriko, maporomoko Hanang

Spread the loveWaathirika wa maporomoko ya tope Wilayani Hanang, mkoani Manyara, waliopoteza...

Habari Mchanganyiko

TPF-NET Arusha yaonya jamii ya wafugaji zinazoendeleza ukatili wa watoto na wanawake

Spread the love  MTANDAO wa Polisi wanawake wa Arusha kuelekea siku 12...

error: Content is protected !!