Thursday , 2 May 2024
Home Kitengo Maisha Afya Magonjwa yasiyoambukiza yanavyoigharimu NHIF
Afya

Magonjwa yasiyoambukiza yanavyoigharimu NHIF

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga
Spread the love

 

WAGONJWA wanaougua magonjwa yasiyoambukiza wametajwa kuwa ndiyo kundi ambalo linatumia fedha nyingi kutoka katika Mfuko wa Bima ya Afya Tanzania (NHIF). Anaripoti Erasto Masalu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yameelezwa leo tarehe 11 Agosti, 2022 na Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Bernard Konga alipokutana na wadau wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema kwa mwaka 2021/22 wagonjwa wa magonjwa yasiyoambukiza wametumia jumla ya Sh. 99.9 bilioni.

Konga amesema katika wanachama 4,821,233 wa NHIF, kati yao wenye magonjwa yasiyoambukiza wamekuwa wakitumia gharama kubwa ukilinganisha na magonjwa mengine hasa katika vipimo, kumuona daktari ikiwa pamoja na dawa zake.

Amesema mfano matibabu ya kusafisha damu kwa mgonjw awa figo kwa mwaka wa 2021/22 imegharibu jumla ya Sh. 35.4 bilioni huku mabongwa mengine yakitumia kiwango kilichobaki katika Sh. 99 bilioni.

“Tunaunga mkono mapambano ya Serikali kupunguza wimbi la magonjwa yasiyoambukizwa kwani yamekuwa tishio kwa sasa, kutokana na kuwashambulia watu wengi, lakini pia kwa matibabu yake nayo yana gharama kubwa sana.

“Gharama za kusafisha damu kwenye figo, inagharimu karibu ya Sh. 250,000 mara moja na ndani ya wiki mgonjwa anatakiwa kufanyiwa vipindi vinne, hapo utaweza kupata picha ni kiasi gani kinatakiwa. Fikiria mtu huyo akiwa hana Bima ya Afya, atawezaje kumudu matibabu hayo,” alisema Konga.

https://youtu.be/I4L-B6dvQIA

Wakati huo huo, Konga amesema wanaendelea kufanya maboresho katika maeneo mbalimbali ya mfuko huo, katika vipimo, matibabu na dawa kwa lengo la kudhibiti udanganyifu unaotokea mara kwa mara.

“Kila huduma zina changamoto zake, moja ya mambo ambayo tunkutana nayo ni pamoja na udanganyifu kwa watoa huduma, hivyo maboresho haya yanaenda kuondoka udanganyifu huo ikiwa pamoja na kuondoa usumbufu wa mgonjwa na kulinda afya yake kwa ujumla,” alisema Konga na kuongeza:

“Unaweza kukuta mgonjwa anatibiwa leo hospitali hii, kesho nyingine, keshokutwa nyingine kwa daktari yule yule, maboresho haya yanaenda kuondoa tatizo hilo.”

Konga amesema; “Tumeweka utaratibu baadhi ya vipimo lazima kuwe na kibali kutoka NHIF, hii itasaidia kwa watoa huduma kuwaandikia kiholela wagonjwa kwa lengo la kuingiza fedha, mfano MRI, Ecko na vipimo vingine vikubwa.”

Mkurugenzi huyo pia amesema pia maboresho mengine ni mfumo wa bei mpya za dawa ambapo mpaka ifikapo Novemba 1, 2022 itakuwa na bei mpya ambazo zitalenga kukabiliana na utapeli pamoja na udanganyifu unaofanywa na baadhi ya watoa huduma na hivyo kutishia kuingizia hasara mfuko huo.

Aidha Konga amesema kuwa katika wanachama wake 4,821,233 ambao ni sawa na 8% ya Watanzania wote ambao wamegawanyika katika makundi matatu, watumishi wa Umma, Mfuko wa Bima kwa wote na wBima binafsi.

Konga amesema katika makundi hayo matatu, kundi la Bima Binafsi ambao ni 1% ya wanachama wote wa NHIF wamekuwa changamoto kubwa kwani wamekuwa wakijiunga kwa uchachi hali inayosababisha huduma zao zimekuwa na shida.

Amesema wanachama wa Bima Binafsi hadi sasa ni 48,000 ambayo idadi chache na wengi wao wamejiunga baada ya kugundua kuwa wanasumbuliwa na maradhi Fulani, hali ambao si afya kwa mfuko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

Songwe katika mikakati ya elimu ya lishe kudhibiti udumavu

Spread the love  SERIKALI mkoani Songwe imejipanga kuendelea kutoa elimu ya lishe...

Afya

Mloganzila yajipanga kupandikizaji wa ini

Spread the love  HOSPITALI ya Taifa Muhimbili-Mloganzila imesema kutokana na uwekezaji uliofanywa...

AfyaHabari za Siasa

Serikali yasaka watumishi afya ngazi ya jamii 8,900

Spread the loveSERIKALI imeanza utekelezaji wa mpango jumuishi wa wahudumu wa afya...

AfyaHabari za SiasaTangulizi

Bima ya afya kwa wote kuanza Aprili, wajane kicheko

Spread the loveSHERIA ya Bima ya Afya kwa Wote, inatarajiwa kuanza kutumika...

error: Content is protected !!