Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Mbunge wa Makambako aishukuru Serikali uboreshaji huduma za kijamii
Habari za Siasa

Mbunge wa Makambako aishukuru Serikali uboreshaji huduma za kijamii

Spread the love

 

MBUNGE wa jimbo la Makambako nchini Tanzania, Deo Sanga, amesema kujengwa kwa vituo vya afya takribani vitano katika halmashauri ya wilaya ya Makambako kumerahisisha upatikanaji wa huduma bora za afya kwa wananchi wa halmashauri hiyo. Anaripoti Felister Mwaipeta, TUDARCo … (endelea).

Mbunge huyo ameyasema hayo leo Alhamisi tarehe 11, Agosti, 2022, wakati akihutubia wananchi wa Makambako akiwa kwenye msafara wa Rais Samia Suhulu Hassan ambaye anaelekea mkoani Iringa kwa ziara ya kikazi.

Sanga amesema wilaya ya Makambako awali kulikuwa na kituo kimoja tu cha afya ambacho ni kituo kikuu cha Makambako na kwamba kwa sasa kuna vituo takribani vitano ambavyo ni lyamkena, Itelu, Mahonge na kituo cha Utengule.

Katika suala la elimu Mbunge Deo amekiri kujengwa kwa madarasa zaidi ya 11 katika shule za msingi na sekondari sambamba na ujenzi wa mabweni katuika shule za sekondari tano.

Amesema awali kulikuwa na changamopto ya uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo kila shule ya msingi na sekondari ilikuwa na madarasa mawili.

Mbunge Deo aliendelea kuipongeza Serikali kwa utekelezaji wa hali ya juu wa miradi kwa kuhakikisha upatikanaji wa miundombinu ya umeme katika vijiji mbalimbali vya halmashauri ya Makambako.

“Uwepo wa miundo mbinu bora ya barabara katika halmashauri ya Makambako imechangia katika kukuza uchumi wa wananchi ukilinganisha na hapo awali,” amesema Sanga.

Aidha mbunge huyo amemuomba Rais Samia kujengwa kwa soko kuu la kisasa kama lile la mkoa wa Njombe pamoja stendi ya kisasa ya mabasi ya kwenda mikoani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

CCM yakemea ufisadi, yaipa kibarua TAKUKURU

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimekemea vitendo vya ubadhirifu wa...

Habari za Siasa

Bajeti ya Ikulu 2024/25 kuongezeka, bunge laombwa kurudhia Sh. 1.1 trilioni

Spread the love  WIZARA ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa...

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

error: Content is protected !!