JESHI la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam limewaonya Mashabiki wa Soka nchini watakaokwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mchezo wa Ngao ya Jamii utakaopigwa Jumamosi tarehe 13 Agosti, 2022 na kuwakutanisha watani wa jadi, wasiende na silaha ya aina yoyote. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Mabingwa wa Soka Tanzania Bara, Young Africans watapapatuana na Simba SC katika mchezo huo ambao utatumika kama ishara ya ufunguzi wa Msimu Mpya 2022/23.
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 11 Agosti, 2022 Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Muliro Jumanne Muliro amesema shabiki yoyote hataruhusiwa kwenda Uwanja wa Benjamin Mkapa akiwa na silaha isipokuwa vyombo vya dola.
“Katika kuelekea mchezo huo, Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam litachukua tahadhari zote za kiusalama kabla, wakati na baada ya mchezo, usalama utaimarishwa kwa kiwango cha juu”
“Ni marufuku kwa Mtu yeyote kwenda na silaha uwanjani isipokuwa vyombo vya dola vyenye jukumu la usalama eneo hilo, tunawatoa hofu Mashabiki watakaofika kushuhudia mchezo huo kuwa ulinzi ndani na nje ya uwanja utakuwa umeimarishwa kwa kiwango cha juu” amesema Kamanda Muliro
Leave a comment