Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko LSF yanoa mashirika yanayosimamia watoa misaada ya kisheria
Habari Mchanganyiko

LSF yanoa mashirika yanayosimamia watoa misaada ya kisheria

Spread the love

SHIRIKA la Legal Services Facility (LSF), linaendesha kikao cha kuzijengea uwezo mashirika takribani 92 yanayosimamia wasaidizi wa kisheria kwenye kanda zake sita nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam…(endelea).

Kikao hicho cha siku mbili kuanzia jana na leo Ijumaa, tarehe 10 Februari 2023, kinafanyika jijini Dar es Salaam, kwa ajili ya kuongeza ubora, uwezo na maendeleo ya kitaasisi katika kutoa huduma za msaada wa kisheria kwenye jamii.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi hicho, Meneja Programu LSF, Wakili Deogratias Bwire, amesema kinalenga kujenga uelewa wa pamoja miongoni mwa watendaji wa mashirika simamizi (ZMOs), kwa ajili ya kuonesha uelekeo mzuri wa utekelezaji programu ya upatikanaji haki nchini na kuleta matokeo tarajiwa kulingana na miongozo ya LSF ikiwemo mpango mkakati wa miaka mitano pamoja na Mpango wa Taifa wa Maendeleo.

“Kikao hiki kinafanyika ili kukidhi mahitaji ya mabadiliko ya mfumo wa utekelezaji wa programu yetu ya upatikanaji wa haki nchini hasa katika utoaji wa ruzuku. Awali, LSF ilikuwa na mfumo wa kutoa ruzuku kwa mashirika ya wasaidizi wa kisheria kupitia mashirika simamizi na baadae iliamua kutoa ruzuku moja kwa moja. Sasa tumeamua kuwa na usimamizi wa kikanda ili kuongeza ufanisi zaidi,” amesema Bwire.

Meneja wa Usimamizi na Matokeo LSF, Said Chitung, amesema kuwa kikao hicho kinalenga kuongeza usimamizi wa programu kwa kujenga uwezo kwa mashirika ya msaada wa kisheria ambayo ZMOs watayasimamia katika kanda zao.

“ZMOs hawa kazi yao kubwa ni kufanya usimamizi wa programu ya LSF katika mikoa mbalimbali ambayo watakwenda kuisimamia kulingana na kanda zao tulizowapa. Tunategemea mfumo huu utupe matokeo makubwa zaidi mwisho wa programu yetu kama tulivyokubaliana katika kikao hiki muhimu,” amesema Chitung.

Naye Afisa wa Fedha kutoka Shirika la Morogoro Paralegal Centre (MPLC), Regina Solomon ameeleza kuwa ,kikao kimesaidia kujenga uelewa wa pamoja katika utoaji wa taarifa (reporting) zenye matokeo kuhusu utekelezaji wa mradi katika maeneo ambayo ZMOs atakwenda kuyasimamia chini ya ufadhili wa LSF.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali yapunguza kodi ya makampuni kwa 20%

Spread the loveSERIKALI imepunguza kodi ya makampuni kwa asilimia 20, kutoka asilimia...

Habari Mchanganyiko

Mradi uliotaka kumng’oa madarakani Dk. Mpango waanza majaribio

Spread the loveMRADI wa maji wa Mwanga-Same-Korogwe, ambao Makamu wa Rais, Dk....

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Madiwani Msalala wampa tano DED kwa kuongeza mapato

Spread the loveMKURUGENZI wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala, mkoani Shinyanga, Khamis...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kimbunga Hidaya chaua 5, kaya 7,027 zikikosa makazi

Spread the loveSERIKALI imetoa tathmini ya athari za kimbunga Hidaya, kilichotokea tarehe...

error: Content is protected !!