Monday , 6 May 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Kamati ya Bunge yaombwa kuchunguza mauaji wananchi, askari Serengeti
Habari za Siasa

Kamati ya Bunge yaombwa kuchunguza mauaji wananchi, askari Serengeti

Ester Matiko, Mbunge asiye na Chama
Spread the love

MBUNGE Viti Maalum, Esther Matiko, amemuomba Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, aagize Kamati ya Kudumu ya mhimili huo ya Ardhi, Maliasili na Utalii, iende katika Hifadhi ya Serengeti, ili kubaini kama kuna mgogoro unaosababisha mauaji ya wananchi na askari wa hifadhi au lah. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Matiko ametoa ombi hilo leo Ijumaa, tarehe 10 Februari 2023, baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Pindi Chana, kulieleza Bunge kuwa hakuna mgogoro kati ya wananchi wanaoishi kwenye vijiji vinavyozunguka katika hifadhi hiyo.

Aidha, Balozi Chana alidai kuwa awali kulikuwa na changamoto ya baadhi ya wananchi kuwashambulia kwa mishale yenye sumu askari wa hifadhi hiyo, ambapo Serikali imekemea vitendo hivyo.

Kufuatia majibu hayo, Matiko alihoji kama hakuna mgogoro na kuna amani katika maeneo hayo kwa nini mauaji yanatokea.

“Kama hakuna mgogoro kuna amani, haitatokea hata siku moja watu wakarushiana mishale au bunduki, juzi wakati naibu waziri akimjibu Mwita Waitara alivyoomba Serikali ikatatue mgogoro alikiri ataenda kutatua mgogoro. Kwa nini kamati yako isiende ikajiridhishe kama kuna mgogoro au hakuna mgogoro ili kutatua,” amesema Matiko.

Akijibu ombi hilo, Spika Tulia amesema mwaka jana Bunge liliipa Serikali miezi mitatu kufanyia kazi malalamiko yaliyotolewa na wabunge kuhusu mgogoro huo kisha kuwasilisha taarifa bungeni jijini Dodoma.

Spika Tulia amesema taarifa hiyo ilipaswa kuwasilishwa bungeni Septemba 2023, lakini imechelewa kuwasilishwa ili ifanyiwe marekebisho katika baadhi ya mapungufu yaliyojitokeza.

Amesema, taarifa hiyo inatarajiwa kuwasilishwa bungeni katika Bunge la Bajeti Juni 2023, kisha mhimili huo utajiridhisha kama kuna haja ya kutuma kamati hiyo kubaini kama kuna mgogoro au la.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Jacob, Malisa wapandishwa kizimbani kwa mashtaka ya uongo mitandaoni

Spread the loveMKURUGENZI wa Shirika la Haki, Godlisten Malisa na mwanachama wa...

BiasharaHabari za Siasa

Bunge laitaka Serikali kudhibiti ufisadi miradi ya mkakati

Spread the loveKAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, imeitaka Serikali kuimarisha...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wizara ya Uchukuzi yaomba kuongezewa bajeti na Bunge

Spread the loveWIZARA ya Uchukuzi imeliomba Bunge liidhinishe bajeti yake kwa mwaka...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Serikali kutafuta mwekezaji mwingine Bandari ya Dar es Salaam

Spread the loveSERIKALI inaendelea kutafuta mwekezaji mwingine atakayeendesha gati namba nane hadi...

error: Content is protected !!