Thursday , 9 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Dk. Tax asaini kitabu cha Maombolezo ubalozi wa Uturuki
Habari Mchanganyiko

Dk. Tax asaini kitabu cha Maombolezo ubalozi wa Uturuki

Spread the love

WAZIRI wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stergomena Tax, amesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa Uturuki Jijini Dar es Salaam, kutokana na maafa yaliyosabishwa na tetemeko la ardhi lililotokea Uturuki tarehe 6 Februari 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu.. (endelea)

Baada ya kusaini kitabu cha maombolezo, Dk. Tax ametoa salamu za pole kwa Serikali ya Uturuki na kuwasihi kuendelea kuwa wavumilivu wakati huu wa msiba mkubwa kwa Taifa hilo uliosabaisha vifo vya watu zaidi ya 18,000.

“Serikali ya Tanzania na Watanzania kwa ujumla tunaungana na Serikali ya Uturuki katika kuombeleza msiba huo mzito,” alisema Dkt. Tax.

Mwaka 1999 Uturuki ilikumbwa na tetemeko la ardhi ambapo watu wapatao 17,000 walipoteza maisha kutokana na tetemeko hilo. Kadhalika, mwaka 2011 ilikumbwa na tetemeko la ardhi katika mji wa Van lilipelekea vifo vya watu 500.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

DAWASA yatekeleza agizo la Samia kwa kutangaza zabuni kielektroniki

Spread the loveKiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa, Godfrey Mnzava...

Habari MchanganyikoMichezo

Kengold wakabidhiwa kombe NBC Championship

Spread the loveMdhamini mkuu wa Ligi Daraja la Kwanza (NBC Championship) Benki...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia: Matumizi ya nishati safi sio anasa, ladha ipo

Spread the loveRAIS Samia Suluhu Hassan amesema matumizi ya nishati safi kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC, SILABU waungana kufikisha elimu ya fedha majumbani

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeingia makubaliano ya ushirikiano...

error: Content is protected !!