Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atoa angalizo “siku zijazo hazitakuwa rahisi”
Habari za Siasa

Lissu atoa angalizo “siku zijazo hazitakuwa rahisi”

Tundu Lissu, Makamu Mwenyekiti wa Chadema
Spread the love

 

MAKAMU Mweneykiti wa Chadema Bara, Tundu Lissu amesema siku zijazo hazitakuwa rahisi licha ya ahadi ya Rais Samia Suluhu Hassan na utayari wa chama chake katika katika kufikia maridhiano ya kisiasa. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

“Ninafahamu kwamba licha ya ahadi ya Mh. Rais na licha ya utayari wangu na wetu kama chama, siku zijazo hazitakuwa rahisi. Ninajua kuwa tutakabiliwa na majaribu ya kila aina na tutapitishwa katika tanuru kubwa la matatizo na magumu mengi,” amesema Lissu leo Ijumaa tarehe 13 Januari, 2023, katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya.

Hata hivyo amewapa moyo wafuasi wao “licha ya mazingira hayo magumu na mbele ya changamoto kubwa na nyingi zitakazotukabili ninaamini kwamba kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yeremia, Mwenyezi Mungu anatuwazia sisi Watanzania mawazo yakutustawisha na wala sio ya kutubomoa, mawazo ya kutupa tumaini katika siku zetu zijazo.”

“Ninarudi kwaajili ya kazi kubwa iliyopo mbele yetu, kazi ya Katiba Mpya na mwanzo mpya kwa Taifa letu, ninarudi nyumbani kuja kushiriki katika kuandika ukurasa wa kwanza mpya wa kitabu chenye kurasa 365 cha mwaka huu 2023,” amesema Lissu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!