February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Korea washangilia bomu la Nyuklia

Moja ya kombora la Korea Kaskazini baada ya kurushwa

Spread the love

KOREA Kaskazini imefanya sherehe kubwa kwa ajili ya kuwaenzi wanasayansi waliofanikisha majaribio makubwa ya bomu la Nyuklia nchini humo, anaandika Irene Emmanuel.

Sherehe hiyo imefanyika katika Mji Mmkuu, Pyongyang huku wananchi wakishangilia wanasayansi waliokuwa ndani ya basi katika barabara kuu za mji huo.

Wananchi walijumuika katika Uwanja wa Kim II-Sung yu kuwapongeza wanasayansi hao.
Siku ya Jumapili Korea Kaskazini ilifanyia jaribio kwa mafanikio bomu la Nyuklia aina ya Hydrogen lenye uwezo wa kufanya uharibifu.

Hili ni jaribio la sita kuhusu majaribio ya Nyuklia nchini humona kwamba lilisababisha mtetemeko wa ardhi wenye ukubwa wa 6.3 kwa kipimo cha rishta.

Korea Kaskazini imefanya jaribio hilo licha ya taharuki kutanda katika Peninsula ya Korea na vikwazo vya kila mara kutoka Marekani na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa dhidi yake.

Serikali ya Korea Kaskazini inasisitiza kuwa inalazimika kumiliki silaha za Nyuklia kwa lengo la kujihami kutokana na vitisho vya Marekani vya kuivamia kijeshi kwa mabomu.

error: Content is protected !!