February 25, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Wakimbizi wa Burundi waanza kurejea kwao

Spread the love

AWAMU ya kwanza ya wakimbizi wa kutoka Burundi wanaorejea kwa hiari yao kutoka Tanzania wanatarajiwa kuwasili nchini mwao hii leo, anaandika Jovina Patrick.

Hatua hiyo imefikiwa baada ya makubaliano wiki iliyopita kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR), Tanzania na Burundi.

Abel Mbilinyi, Mwakilishi Mkazi wa UNHCR nchini Burundi amethibitisha kurejea kwa wakimbizi 300 nchini humo.

Wakimbizi hao wanafuikia katika vinne vilivyo katika maeneo ya mashariki na kusini mwa Burundi pamoja na mji mkuu Bujumbura.

Inakadiriwa kwamba hadi kufikiab mwisho wa mwaka huu, wakimbizi 12,000 wa Burundi wanaoishi Tanzania watakuwa wamerejea kwao.

Kuna wakimbizi takribani 250,000 wa Burundi katika kambi mbali mbali hapa nchini.

error: Content is protected !!