February 28, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mgombea urais Tanzania atupia lawama Polisi

Hashim Rungwe, Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chauma)

Spread the love

ALIYEKUWA mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hashim Rungwe ametupia lawama Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwamba limemuonea kwa kumkamata usiku, anaandika Faki Sosi.

Rungwe ambaye pia Mwenyekiti wa Chama Cha Ukombozi wa Umma (Chauma) amesema hana kosa lolote lakini alikamatwa na Polisi na kuwekwa ndani kwa siku kadhaa.

Akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa, polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam hawakumtendea haki kutokana na kumkamata usiku nyumbani kwake ilhali aliwapa vielelezo vyote kuhusu kusaini kwa mkataba wa biashara kati ya mfanyabiashara wa Uturuki na Tanzania.

Rungwe amekiri kuhusika na mkataba huo kutoka kwa wateja wake kwa kufuata sheria na kwamba alimpelekea pesa hizo mfanyabiashara wa kitanzania ili atimize makubaliono na mfanyabiasha wa uturuki.

error: Content is protected !!