Tuesday , 27 February 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Tundu Lissu apigwa risasi Dodoma, viongozi wanena
Habari za SiasaTangulizi

Tundu Lissu apigwa risasi Dodoma, viongozi wanena

Tundu Lissu, Mbunge wa Singida Mashariki, akilia kwa uchungu
Spread the love

NI taharuki, vilio na simanzi katika hospitali ya mkoa wa Dodoma, baada ya Tundu Lissu, Mwanasheria Mkuu wa Chadema na MBunge wa Singida Mashariki, kuvamiwa na watu wasiojulikana na kupigwa risasi za tumbini na mguuni, anaandika Dany Tibason.

Wananchi, wanachama wa Chadema, Wabunge, Naibu Spika, Katibu wa Bunge na watu wengine walifulika hospitalini hapo kwa lengo la kujua maendeleo ya afya ya mbunge huyo.

Lissu amevamiwa nyumbani kwake na watu wasiojulikana majira ya saa saba na nusu mchana akiwa ndani ya gari akitokea bungeni.

Kauli ya Mbowe

Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akizungumza na wananchi pamoja na waandishi wa habari katika hospitali ya mkoa.

Mbowe amesema kuwa Chadema pamoja na jamii kwa ujumla wamesikitishwa na kitendo kilichofanyika kwa shambulizi lililofanywa dhidi ya Lissu.

Amesema ni taswira mbaya kwa taifa kuona viongozi wakishambuliwa tena mchana kweupe huku kukiwa na vyombo vya ulinzi na usalama.

Hata hivyo amesema kitendo ambacho kimefanywa kwa kumshambulia Lissu kinatakiwa kutodhalauliwa na vyombo vya ulinzi na usalama vifanye uchunguzi wa kina na kutoa ripoti.

Hata hivyo amewaomba wananchi kuwa watulivu wakati mbunge huyo akiendelea kupatiwa matibabu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma

Jordan Lugimbana, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ametangaza kuzuia mikusanyiko ya watu ili kuimalisha usalama zaidi.

Lugimbana amesema kuwa kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na msako ili kuweza kuwabaini watu waliohusika na uharifu.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari Lugimbana amesema majira ya saa saba na nusu, Lissu akiwa anatokea bungeni wakiwa amefika nyumbani kwake kabla hajatelemka katika gari lake alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.

Mganga Mkuu

Akizungumza na waandishi wa habari mganga mkuu wa mkoa wa Dodoma, James Kihologwe amesema kuwa afya ya Lissu inaendelea vizuri.

Mbali na hilo amesema kuwa jopo la madaktari wanaendelea kumpatia huduma za matibabu.

Kamanda wa Polisi Mkoa

Naye Kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma, Gells Mroto amesema kuwa kwa sasa jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi na kwa sasa barabara zote za Dodoma -Dar es salaam, Dodoma -Singida, Dodoma -Irinda na Dodoma -Kondoa.

Amesema uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na watakaokamatwa watatiwa nguvuni na hatua za kisheria zitachukuliwa.

Katibu wa Bunge

Dk. Thomasi Kashilla, Katibu wa Bunge amesema kwa sasa anatibiwa kwa bima ya Bunge lakini ikifikia hatua kutibiwa nje ya nchi Bunge litahusika.

Waziri wa Mambo ya Ndani

Naye Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amesema kuwa serikali pamoja Wizara kwa ujumla wanalaani kitendo cha kumshambulia Lissu kwa Risasi.

Mbali na kulaani amesema ameagiza jeshi la polisi kuwasaka waalifu kwa njia yoyote.

“Nimeagiza polisi wawasake waharifu na kufunga njia zote zilizo rasmi na zisizokuwa rasmi, kilichotendeka hakikubaliki iwe hira, siasa, ugomvi, hujuma au uhalifu tutapambana naye.

“Tunalaani kuwashambulia viongozi tena jua kali mchana kweupe,” amesema Mwigulu.

Ummy Mwalimu

Naye Waziri Afya, Ustawi wa Jamii, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu amesema kuwa kwa sasa hali ya mgonjwa inaendelea vizuri kwani hatua ya kwanza imeimalika na sasa inafuatia hatua ya pili ya matibabu.

Hata hivyo amesema kwa sasa wanasubiri ushauri wa jopo la madaktari ili kuona kama wanaweza kumsafirisha kwenda hospitali ya Rufaa Muhimbili au la.

Spika wa Bunge, Job Ndugai

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema kuwa alipata taarifa za tukio baada ya kumalizika kwa makabidhiano ya tume ya Almasi na Tanzanaiti.

Hata hivyo amesema bunge litahakikisha linatia msaada wa aina yoyote kwa Lissu kadri itakavyohitajika ili afya yake iweze kuimarika.

Amewaomba wapiga kura wake kuwa wavumilivu na kumuomba Mungu ili amponye haraka.

Hali ya hospitali

Wananchi wa mkoa walifulika hospitalini hapo kwa lengo la kumjulia hali mbunge huyo jambo ambalo limepelekea uongozi wa hospitali kuzuia watu wasiingie.

Gari la Tundu Lissu likiwa limetobolewa kwa risasi

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Hamahama Ngorongoro kutikisa maandamano ya Chadema Arusha

Spread the loveMAELFU ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Demokrasia na...

Habari za SiasaTangulizi

Waliofariki ajalini Arusha kuagwa siku ya maandamano Chadema

Spread the loveMIILI ya watu 25 waliofariki dunia katika ajali iliyohusisha lori...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali kuiburuzwa mahakamani ajali iliyoua 25 Arusha

Spread the loveMTANDAO wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC), imeitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Samia atoa pole ajali iliyoua 25, kujeruhi 21 Arusha

Spread the loveRais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Mkuu...

error: Content is protected !!