Tuesday , 7 May 2024
Home Kitengo Biashara Kikwete aipongeza NBC kwa ukuaji, ushirikiano na wateja
BiasharaHabari Mchanganyiko

Kikwete aipongeza NBC kwa ukuaji, ushirikiano na wateja

Spread the love

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Kikwete ameelezea kuridhishwa kwake na kasi ya ukuaji pamoja na uimara wa taasisi za fedha hapa nchini huku akizisisitiza taasisi hizo kuendelea kujiendesha kwa weledi zaidi ili ziweze kuongeza tija katika kuchochea ongezeko la uwekezaji na ukuaji wa uchumi wa nchi kupitia sekta mbalimbali ikiwemo biashara. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akizungumza kwenye hafla fupi ya futari iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Dk. Kikwete aliitumia benki ya NBC kama mfano muhimu katika kuthibitisha uimara wa taasisi hizo ambazo pamoja na kuongeza viwango vya mikopo na huduma mbalimbali kwa wateja pia zimeweza kutengeneza faida kubwa na hivyo kuendelea kijiimarisha zaidi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete (kushoto) akipokea zawadi maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (kulia) wakati wa hafla futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake wa jijini Dar es Salaam jana. Hafla hiyo ilifanyika jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

“Ninapotoa pongezi na shukrani naamanisha kwa dhati kabisa kwa sababu mabadiliko mengi ya taasisi ya kifedha yalifanyika mimi nikiwa Waziri wa Fedha kwa wakati ule hivyo najua vema tulipo sasa na tulipotoka.

“Leo hii nikiona mabenki yanatangaza faida kwa mabilioni ya fedha yananithibitisha wazi kabisa kuwa zile ‘reforms’ tulizozifanya kipindi kile zimefanikiwa,’’ alibainisha Dk. Kikwete huku akiitolea mfano benki ya NBC iliyotengenza faida ya Sh 122 bilioni kwa mwaka uliopita.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete (katikati walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi waandamizi wa benki ya NBC pamoja na wateja wa benki hiyo jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake jijini humo. Hafla hiyo ilifanyika jana jijini humo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Akitumia mifano na historia zaidi, Dk. Kikwete alitumia muda mwingi kuelezea namna wateja walivyopitia wakati mgumu kupata huduma za kifedha kwenye taasisi hizo kabla ya serikali kuingilia kati na kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo kufunga na kubadili muundo wa uendeshaji na umiliki kwa baadhi ya benki hizo.

‘’Leo hii changamoto zote zimebaki historia. Fedha kwenye Uchumi ndio damu ya Uchumi. Sekta ya fedha ikiteteleka ndio chanzo cha uchumi kuporomoka. Uchumi wa nchi unategemea sekta ya fedha hivyo ikiteteleka kila kitu kinaharibika.

“Hivyo nawapongeza sana NBC na taasisi nyingine zote kwa kuendelea kutoa huduma zenu kwa weledi huku pia mkiendelea kujiimarisha kimitaji,’’ aliongeza.

Akizungumzia matukio ya benki hiyo ya kuandaa futari kwa ajili ya wateja wake kwenye maeneo mbalimbali hapa nchini Dk. Kikwete alisema matukio kama haya yanaongeza imani kwa wateja wa benki hiyo kwa kuwa ni moja ya thibitisho kuwa uhusiano wa benki na mteja haushii kwenye biashara pekee bali pia unagusa imani za wateja.

“Matukio ya futari kama haya yanasababisha wateja wenu tunajisikia vizuri kwa kuwa tunaona kwamba tunahudumiwa na benki ambayo pia inajali maslahi yetu kiimani’’ aliongeza.

Awali akizungumzia hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, alisema ni muendelezo wa utaratibu wa benki hiyo kwa miaka 15 sasa ikilenga kujumuika na wateja wake kama hatua ya kuonyesha mshikamano na umoja katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.

Alisema benki hiyo inaheshimu sana Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kutokana na ukweli kwamba, ni kipindi ambacho mwanadamu anajiweka karibu na Muumba wake kupitia mfungo na kufanya maombi.

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete (pichani) akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya NBC kwa ajili ya wateja wake jijini Dar es Salaam.

“Huu ni mwezi ambao pia unatukumbusha kufanya kilicho chema mbele za Mungu wetu. Kwa kuwa NBC siku zote tupo karibu imani za wateja wetu tumeamua kuandaa futari hii ili kujumuika na wenzetu kufanikisha hilo,” alisema Sabi.

Zaidi Sabi aliangazia huduma maalum ya benki hiyo, “La Riba,” iliyoandaliwa kwa ajili ya wateja wenye imani ya kiislamu kwa kuzingatia kanuni za dini hiyo katika masuala yanayohusiana na fedha na mtazamo wa dini hiyo kuhusiana na riba.

‘’NBC ndio benki ya kwanza kubwa kuanzisha huduma za kibenki zinazozfuata misingi ya kisheria kupitia La Riba Banking ikiwemo akaunti za akiba na biashara kwa watu binafsi, wajasiriamali na makampuni makubwa.

“Benki pia inayo akaunti ya muda maalum (fixed deposit) inayofuata misingi ya sharia yaani ‘Mudharaba’. Zaidi kupitia dirisha hilo la La Riba tunatoa huduma ya mikopo kwa wafanyanyabiashara wakubwa na wa kati, wajasiriamali wadogo na wafanyakazi wa sekta ya umma na sekta binafsi,’’ alibainisha Sabi.

Hafla hiyo ya futari ilihudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo viongozi wa serikali, viongozi wa dini wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Sheikh Walid Alhad Omar, viongozi wa vyama vya siasa, wateja, mawakala pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

Biashara

Cheza kwa kuanzia Sh 400 kushinda mgao wa Expanse Tournament kasino 

Spread the love  UKISIKIA bosi kacheka ujue Maokoto yanafuatia, Kupitia promosheni pendwa...

error: Content is protected !!