Friday , 29 September 2023
Home Kitengo Habari Kimataifa Kesi ya Trump Machi mwakani, mbio za urais shakani
Kimataifa

Kesi ya Trump Machi mwakani, mbio za urais shakani

Trump
Spread the love

KESI dhidi ya rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump kutokana na madai ya kujaribu kuingilia matokeo ya uchaguzi wa rais wa 2020 itaanza kusikilizwa Machi mwaka 2024 katika mahakama ya shirikisho jijini Washington nchini humo. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Tarehe hiyo inatajwa kumuathiri kisiasa katika mbio zake za kuusaka urais wa taifa hilo kubwa duniani hasa ikizingatiwa itasikilizwa siku moja kabla ya uchaguzi wa ndani ya chama chake cha Republican wa kumchagua mgombea Urais.

Jana tarehe 28 Agosti 2023, Jaji Tanya Chutkan ambaye atasikiliza kesi hiyo amethibitisha itaanza tarehe 4 Machi 2024 siku moja kabla ya ‘Super Tuesday’, siku ambayo majimbo 15 hupiga kura za kuteua wagombea wa urais kwenye uchaguzi mkuu.

Takwimu zinaonyesha kwamba kufikia sasa Trump anaongoza miongoni mwa watu wanaonuia kuwania urais kupitia chama cha Repablikan.

Waendesha mashitaka walikuwa wamependekeza kesi hiyo ianze tarehe 2 Januari mwakani, wakati mawakili wa Trump wakiomba isogezwe hadi Aprili 2026, miaka miwili baada ya uchaguzi wa mwaka ujao kufanyika.

Hata hivyo, Jaji Chutkan alikataa mapendekezo hayo, wakati tarehe aliyotaja ikionekana kuathiri kampeni ya Trump, pamoja na kesi nyingi zinazomkabili.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Kimataifa

Wadukuzi wa Kichana waiba barua pepe 60,000 za Serikali ya Marekani

Spread the loveWADUKUZI wa kichana wamedukua barua pepe 60000 serikali ya Marekani...

Kimataifa

Mahakama yamkuta na hatia Donald Trump

Spread the love  ALIYEKUWA Rais wa Marekani, Donald Trump, amekutwa na hatia...

Kimataifa

Harusi yageuka msiba 100 wakifariki kwa ajali ya moto

Spread the love  WATU takribani 100, akiwemo bibi na bwana harusi, wamefariki...

Kimataifa

Kampuni ya mali ya China Oceanwide yapata agizo la kufilisiwa huko Bermuda

Spread the love  MAHAKAMA ya Bermuda imetoa amri ya kufilisiwa kwa Kamapuni...

error: Content is protected !!