Friday , 29 September 2023
Home Habari Mchanganyiko Mwenyekiti wa Bodi ya TMA akagua ofisi, kituo cha tahadhari ya Tsunami
Habari Mchanganyiko

Mwenyekiti wa Bodi ya TMA akagua ofisi, kituo cha tahadhari ya Tsunami

Spread the love

 

MWENYEKITI wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi amekagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania, Kanda ya Mashariki na Kituo cha kutoa tahadhari za TSUNAMI nchini, unaotekelezwa katika maeneo ya SIMU 2,000, Jijini Dar es Salaam. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Mradi huo ambao utagharimu zaidi ya shilingi Bilioni 9 za kitanzania, unatarajiwa kukamilika mwezi Julai,2024.

Akizungumza wakati wa ziara yake, Dk. Nyenzi alisema, chini ya Serikali ya Awamu wa Sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan, mamlaka imekuwa wanufaika wakubwa katika uboreshaji wa huduma za hali ya hewa nchini ukiwemo mradi huo ambao utahusika moja kwa moja katika utoaji wa tahadhari za TSUNAMI nchini na hivyo kuongeza tija katika mipango ya nchi.

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Dk. Buruhani Nyenzi

Aidha, Dkt. Nyenzi alifurahishwa na kasi ya ujenzi unavyoendelea kutokana na hatua mbalimbali ambazo mkandarasi amezichukua ikiwa ni pamoja na kufanya kazi muda wa ziada na kuongeza nguvu kazi ili kuhakikisha makubaliano ya kimkataba yaliyowekwa yanafikiwa kwa wakati.

Dk. Nyenzi alisisitiza matumizi ya malighafi zenye ubora na kutoa fursa za ajira kwa wazawa katika mradi huo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi wa wanawake watakiwa kuchangamkia fursa za elimu

Spread the love  KAMISHNA wa Polisi Utawala Menejimenti ya rasilimali watu, CP...

Habari Mchanganyiko

Vijana 400 waguswa na programu ya “Learning for Life” ya SBL

Spread the love  PROGRAMU ya “Learning for Life” imetimiza dhamira ya Serengeti...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Stamico yafungua fursa za kiuchumi kwa makundi maalumu

Spread the loveSHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) limemwaga neema kwa watu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Maabara ya bilioni 5 upimaji madini yazinduliwa Geita, inapima kwa mionzi

Spread the loveZaidi ya Sh bilioni tano zimewekezwa katika kampuni ya MSALABS...

error: Content is protected !!