Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara Rais Samia azindua ujenzi skuli ya Mil. 600/- inayojengwa na NMB
Biashara

Rais Samia azindua ujenzi skuli ya Mil. 600/- inayojengwa na NMB

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan ameweka Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Skuli ya Maandalizi Tasani, iliyopo Shehia ya Tasani, Makunduchi – Zanzibar inayojengwa na Benki ya NMB kwa gharama  ya Sh. 600 milioni hadi itakapokamilika Disemba 2023. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mradi huo umezinduliwa ikiwa ni sehemu ya Tamasha la Kizimkazi (Kizimkazi Festival 2023), linaloendelea Paje, Mkoa wa Kusini Unguja, visiwani Zanzibar.

Tamasha hilo lililozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, Agosti 26 mwaka huu, linafanyika chini ya kauli mbiu ‘Tuwalinde Kimaadili Watoto Wetu kwa Maslahi ya Taifa,’ na linatumika kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akitoa maelezo ya awali ya mradi huo wa Tasani kwa Rais Samia, Afisa Mtendaji Mkuu wa NMB, Ruth Zaipuna, amesema ujenzi huo ambao ni sehemu ya Programu ya Uwekezaji kwa Jamii (CSI), ni kati ya jitihada za wazi za benki yake katika kumuunga mkono kufanikisha maendeleo ya elimu nchini.


Zaipuna alimueleza Dk. Samia kwamba ujenzi huo utakaojumuisha madarasa matano yatakayochukua wanafunzi 200 kwa mkupuo mmoja, utakamilika Disemba mwaka huu, tayari kwa mwaka wa masomo wa 2024, ambao utaanza Januari mwakani, na kwamba Skuli ya Maandalizi Tasani itakuwa ni shule ya kwanza katika eneo hilo, ikiwa ni ya tatu kwa Makunduchi.

“Ujenzi wa majengo na samani za ndani kama vile viti, meza na madawati, utaigharimu Benki ya NMB Sh  600 milioni ambazo ni sehemu ya faida yetu tunayoitoa kila mwaka kurejesha kwa jamii.

“Mradi huu ulio kwenye eneo la mita za mraba 467, utajumuisha madarasa matano yatakayobeba wanafunzi 40 kila moja, Ofisi ya Mwalimu Mkuu, Ofisi ya Walimu, jiko, vyoo vya walimu, wafanyakazi na wanafunzi, stoo, Mifumo ya Kisasa ya Maji Safi na Majitaka, pamoja na sehemu ya michezo.


“Mheshimiwa Rais, mradi wa Skuli hii ni uthibitisho wa utayari wa NMB kusapoti Serikali ya Tanzania katika juhudi zake za kuboresha Elimu nchini.

“Tunatambua jitihada zako katika Sekta ya Elimu, nasi tukiwa wadau na washirika muhimu, tukaona ni vema kuunga mkono maono yako ya Elimu Bure. NMB tunajivunia kuwa washirika vinara wa hilo, tukiamini Skuli ya Maandalizi Tasani inaweza kuibua wasomi watakaokuja kuwa viongozi wakubwa,” amebainisha Bi. Zaipuna.

Akizungumza baada ya maelezo hayo, Rais Samia aliishukuru Benki ya NMB kwa namna inavyounga mkono jitihada za Serikali yake na ile ya Mapinduzi ya Zanzibar, katika kuboresha mazingira ya watoto kupata elimu, huku akiweka ahadi ya kurudi Tasani Januari mwakani wakati wa kuzindua shule hiyo.

“Tunaishukuru sana Benki ya NMB kwa kuamua kutuunga mkono kwa kufanya hili la Ujenzi wa Skuli hii kwa ajili ya watoto wetu. Nilikuwa hapa mwaka jana kuzindua Ofisi ya Shehia, niko hapa kuweka Jiwe la Msingi la Ujenzi huu na utakapokamilika, nitarudi Januari mwakani kuja kuizindua skuli hii.

“Niwakumbushe Wana Tasani kwamba niliwaahidi kuzifanyia kazi changamoto mbalimbali na huu ndio muendelezo wa hilo. Sisi ni viongozi wenu, na sio watawala wenu. Tuko kazini kila uchao kutatua kero zenu, jukumu lenu ni kushirikiana na Serikali kwa kuwasikiliza viongozi wa ngazi mbalimbali. NMB watapokamilisha, yatunzeni majengo haya muhimu kwa elimu ya watoto wetu,” alimalizia Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yashiriki maadhimisho Mei Mosi Arusha

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imeungana na maelfu ya...

Biashara

Promosheni ya bil 1 kutoka Meridianbet kasino, cheza na ushinde zawadi kubwa

Spread the love  INGIA katika ulimwengu wa zawadi za kushangaza: Jishindie sehemu...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Equity Bank yaendelea kusotea mabilioni ya fedha mahakama rufani

Spread the loveBENKI za Equity ya Tanzania na Kenya, zimeendelea kupambana mahakamani...

error: Content is protected !!