Friday , 29 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Dugange arejea bungeni, amshukuru Rais Samia
Habari za SiasaTangulizi

Dk. Dugange arejea bungeni, amshukuru Rais Samia

Dk. Festo Dugange
Spread the love

HATIMAYE Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Dkt. Festo Dugange leo Jumanne amerejea bungeni na kuendelea na majukumu yake ikiwamo kujibu maswali ya wabunge yaliyoelekezwa kwenye wizara hiyo ikiwa ni mara ya kwanza tangu alipopata ajali tarehe 26 Aprili 2023.  Anaripoti, Isaya Temu. TUDARCo…(endelea).

Dk. Dugange alipata ajali hiyo katika barabara ya Iyumbu, maeneo ya St. Peter Clever jijini Dodoma na kuzua utata kutokana na usiri uliokuwa umeghubika ajali hiyo ambayo pia ilidaiwa kuhusisha na kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).

Akizungumza leo tarehe 29 Agosti 2023 bungeni jijini Dodoma, Naibu Waziri huyo kabla ya kujibu maswali ya wabunge, alisimama mbele ya bunge na kutoa shukrani zake za dhati kwa watu wote waliojitolea kwa hali na mali wakati alipokuwa na changamoto ya kiafya.

Naibu Waziri huyo alichukua muda mrefu kushukuru huku akitaja orodha ya anaowashukuru akianza na Mwenyezi Mungu, Rais Samia, viongozi wakuu wa Serikali akiwemo Makamu wa Rais, waziri Mkuu, Spika wa Bunge, Waziri wa wizara yake, Mawaziri na Wabunge, wananchi wa jimbo lake la Wang’ing’ombe pamoja na mke wake aliyemtaja kwa jina la Alafiza Moses Dugange.

“…nitumie fursa hii ya Bunge Tukufu kumshukuru sana Dk. Samia, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa namna ambavyo ameniwezesha, kwa upendo wake na wema wake, kwangu na Watanzania wote kuniwezesha kupata matibabu na kuweza kurejea katika majukumu yangu, Namshukuru sana Mheshimiwa Rais…,” alieleza Dk Dugange.

Katika ajali aliyopata usiku wa kuamkia tarehe 26 Aprili 2023 na kupelekea kulazwa Hospitalini kwa wiki kadhaa, ziliibuka tuhuma zikimshusisha na kifo cha mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom) ambaye alizikwa Wilaya ya Iramba mkoani Singida.

Utata huo uliilazimu Serikali kuunda timu ya uchunguzi ambao ripoti ilibaini kuwa hakuna ukweli kwenye jambo hilo na kwamba mwanafunzi huyo alipoteza maisha ghafla Moshi mkoani Kilimanjaro alipokuwa amekwenda kuonana na mpenzi wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Serikali yawaangukia viongozi wa dini

Spread the loveSERIKALI imewaomba viongozi wa dini, waendelee kuelimisha wananchi kudumisha amani...

Habari MchanganyikoTangulizi

Afya ya akili yatajwa chanzo kuvunjika ndoa

Spread the loveCHANGAMOTO ya afya ya akili, imetajwa kuwa chanzo cha migogoro...

Habari za Siasa

Azzim Dewji aitaka Serikali iwanyooshe mafisadi

Spread the loveMFANYABIASHARA maarufu nchini, Azzim Dewji, ameitaka Serikali iwachukulie hatua wezi...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Kapinga: Usambazaji umeme vijijini mwisho Desemba 2023

Spread the love  NAIBU Waziri wa Nishati, Judith Kapinga, amesema ifikapo mwezi...

error: Content is protected !!