Saturday , 27 April 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kamati ya siri UN kujadili ombi la Taliban kuhutubia marais
Kimataifa

Kamati ya siri UN kujadili ombi la Taliban kuhutubia marais

Spread the love

 

UMOJA wa Mataifa (UN) umeunda Kamati maalumu ya siri yenye wajumbe tisa kujadili mkanganyiko uliojitokeza kuhusu viongozi wa Serikali Afghanistan wanaopaswa kuhudhuria na kuhutubia Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN) unaoendelea huko jijini New York nchini Marekani. Anaripoti Mwanaharusi Abdallah, TUDARCo … (endelea).

Hatua hiyo imekuja baada ya uongozi wa kundi la wanamgambo wa Taliban wanaoongoza taifa la Afghanistan kuomba kuhutubia mkutano huo, wakati huohuo mwakilishi wa Serikalio iliyong’olewa madarakani aliyepo UN akiwasilisha majina ya viongozi wanaopaswa kuhutubia mkutano huo.

Uongozi mpya wa Afganistan ambao ulingia madarakani tarehe 15 Agosti, 2021, hautambuliki kama mwakilishi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa.

Taarifa iliyotolewa leo na Msemaji wa UN, Stephane Dujarric imesema tarehe 15 Septemba mwaka huu Katibu Mkuu wa Umoja huo, Antonio Gueterres amepokea barua kutoka kwa Mwakilishi wa Serikali ya awali ya Afghanistan, Balozi Ghulam Isaczai iliyotaja viongozi waliopaswa kuhudhuria mkutano huo.

Hata hivyo, siku tano baadae Katibu Mkuu huyo alipokea barua nyingine kutoka kwa Ameer Khan ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje ya nchi iliyojiita Islamic Emirate of Afghanistan yaani Afghanistan akiomba kushiriki katika mkutano huo.

Katika barua hiyo, Waziri huyo alidai serikali ya awali iliyokuwa chini ya Rais Ashraf Ghani imeondolewa madarakani hivyo moja kwa moja mwakilishi wa Afghanistan huko UN yaani Balozi Isaczai hatambuliki kama mwakilishi wa nchi yao.

Aidha, waziri huyo alisema Taliban tayari wamemteua mwakilishi mpya ambaye ni Mohammad Shaheen.

Msemaji huyo amesema kamati maalumu ya siri yenye wajumbe tisa itakaa kujadili mkanganyiko huo ili kupata jawabu la mwakilishi sahihi wa Afghanistani.

Hata hivyo, ratiba ya kikao cha kamati hiyo haijapangwa licha ya kwamba Afghanistani imepanga kuhutubia mkutano hup tarehe 27 Septemba.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

KimataifaTangulizi

Mkuu wa majeshi Kenya afariki, Ruto atangaza maombolezo

Spread the loveRais wa Kenya, William Ruto ametangaza maombezo ya siku tatu...

Kimataifa

Majaji kuamua hatima ya Zuma leo

Spread the loveMajaji nchini Afrika Kusini leo Jumanne wataamua ikiwa rais wa...

Habari za SiasaKimataifa

Spika Afrika Kusini ajiuzulu kwa tuhuma za rushwa

Spread the loveSpika wa Bunge la Afrika Kusini, Nosiviwe Mapisa-Nqakula ametangaza kujiuzulu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Tetemeko la ardhi laua 7, lajeruhi 800 Taiwan

Spread the loveWatu wapatao saba wamefariki dunia na wengine zaidi ya 800...

error: Content is protected !!