Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Kagame: Nipo tayari kuendelea kuongoza kwa miaka 20 zaidi
KimataifaTangulizi

Kagame: Nipo tayari kuendelea kuongoza kwa miaka 20 zaidi

Spread the love

RAIS wa Rwanda, Paul Kagame amesema kwamba haoni shida yoyote akiendelea kuongoza Rwanda kwa miaka mingine 20, na kuashiria kwamba atagombea muhula mwingine madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2024. Anaripoti Mwandishi Wetu kwa msaada wa mitandao… (endelea).

Kagame, mwenye umri wa miaka 64, ametawala Rwanda kwa zaidi ya miongo miwili. Amesema kwamba anajiandaa kwa muhula mwingine madarakani.

Katika mahojiano na shirika la Habari la Ufaransa France 24, juzi tarehe 8 Julai, 2022, Kagame amesema kwamba “nafikiria kuendelea kuongoza kwa miaka mingine 20. Sina shida na hilo. Uchaguzi unahusu watu kufanya maamuzi kuhusu wale wanaotaka wawe viongozi wao.”

Kagame alishinda uchaguzi wa mwaka 2017 kwa asilimia 99 ya kura zilizopigwa baada ya kubadilisha katiba na kuondoa kikomo cha mihula miwili kwa wagombea urais.

Mabadiliko hayo yalimuongezea Kagame muda wa kutawala Rwanda kwa muhula mwingine wa miaka 7.

Muhula wake wa sasa wa miaka 7 utakapokamilika, Kagame atakuwa na haki kisheria kugombea tena mihula mingine miwili ya miaka 5, kulingana na mabadiliko ya katiba yaliyofanywa.

Hatua ya kubadilisha katiba, ilitoa fursa kwa Kagame kuanza upya utawala wake na kupata nafasi ya kutawala Rwanda hadi mwaka 2034.

Kagame alikuwa na umri wa miaka 36 alipoongoza chama chake cha Patriotic Front na kuwaondoa madarakani viongozi wa Kihutu wanaotuhumiwa kwa mauaji ya karibu watu 800,000 wengi wao wakiwa Watutsi kati ya mwezi Aprili na Julai mwaka 1994.

Paul Kagame alizaliwa mwezi Oktoba mwaka 1957, kusini mwa Rwanda. Familia yake ilikimbia mapigano ya kikabila mwaka 1960 na kuingia Uganda, ambapo aliishi kwa muda wa miaka 30 kama mkimbizi.

Aliungana na rais wa Uganda, Yoweri Museveni na kuanzisha vita vilivyomwezesha Museveni kuingia madarakani, kabla ya Kagame kupewa cheo cha juu katika jeshi la Uganda chini ya utawala wa Rais Museveni.

Alirudi nchini Rwanda mwaka 1990 na kuongoza chama cha Rwandan Patriotic Front RPF katika vita vya miaka 4 hadi Julai 1994.

Chama cha RPF kilianza juhudi za kuleta umoja na maridhiano, ujenzi wa taifa, maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Paul Kagame aliteuliwa kuwa naibu wa rais na waziri wa usalama katika serikali ya umoja wa kitaifa Julai 19,1994.

Alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama cha RPF miaka minne baadaye. RPF kilikuwa sehemu ya serikali ya umoja wa kitaifa.

April 22, 2000, alichukua uongozi kama rais wa Jamhuri ya Rwanda baada ya kuchaguliwa na baraza la mpito na kushinda uchaguzi mkuu wa kwanza wa kidemokrasia kuwahi kuandaliwa nchini Rwanda mnamo mwaka 2003. Alichaguliwa kwa muhula wa pili wa miaka 7, mwaka 2010.

3 Comments

  • Duh!
    Kageuza nchi kuwa mali yake. Atakufa siku moja na nchi itachafuka tena.
    Hajafanikiwa kuwaunganisha wanyaruanda.
    Poleni sana.
    Shida ya viongozi wengi wa Afrika, hawajui namna ya kujenga mfumo wa kitaasisi wa kustaafu kwa amani na kukabidhi nchi.

  • Wakati mwingine tafsiri ya demokrasia si lazima sana ifanane na ya kimagharibi tunapaswa tuwe na demokrasia kwa mkitadha wa sehemu husika wakati mwingine tunapochagua viongozi kila baada ya miaka 5 tunaweza poteza viongozi bora kisa tu miaka mitano imeisha ya yeye kukaa darasani.Ni vizuri tukafikiria kuwa demokrasia kutokana na mazingira ya kila nchi husika
    Sioni tatizo kama wananchi wa Rwanda wameridhia aendelee kutawala Rais Kagame

  • badala ya neno darasani hapo juu kwenye coment yangu naomba lisomeke madarakani

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

Habari za SiasaKimataifa

Mwanamke Rwanda ataka kupambana tena na Kagame

Spread the loveKIONGOZI wa kihistoria wa upinzani nchini Rwanda, Victoire Ingabire Umuhoza,...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari za SiasaTangulizi

Serikali yaanza msako wanaotoa mikopo kausha damu

Spread the loveSERIKALI imeanza kufuatilia watu, vikundi na taasisi zinazotoa kinyume cha...

error: Content is protected !!