Saturday , 20 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mufti: Sensa ni msingi mkuu wa maendeleo
Habari Mchanganyiko

Mufti: Sensa ni msingi mkuu wa maendeleo

Spread the love

MUFTI wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir, amesema sensa ni msingi mkubwa wa maenndeleo ya mtu na hivyo kutoa wito kwa waislamu wote kushiriki zoezi hilo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Sheikh Zubeir ameyasema hayo leo Jumapili tarehe 10 Julai, 2022, wakati akitoa mawaidha kwenye baraza la Eid Al Adha lililofanyika katika Msikiti wa Mfalme wa Morroco, Muhhamad wa sita jijini Dar es Salaam.

“Kama hakunasensaa hakuna maendeleo mahali  popote, mimi nitastaajabu watu wasiopende sensa wakati dunia nzima inafanya sensa,” amesema Sheikh Zubeir.

Ametolea mifano nchi ya Saudi Arabia “inafanya sensa muda ungeruhusu au ingekuwa natoa muhadhara ningeeleza muda iliyofanya sensa.  Masri  wanafanya sensa kama ukitaka Masheikh waende pale wameandika kuna maelefu hapa kama wewe, hiyo ni sensa,”

“Sheikh wa wapi unakataa sensa unawashinda hata masheikh wa Masri, unawashinda Masheik wa Saudia, kwamba una elimu kubwa kuwashinda.”

“Hapa nina maelezo mengi kuhusu sensa waislamu jitokezeni kuhesabiwa tarehe 23 kwasababu sensa ni maendeleo ya mtu mmoja mmoja hata wewe nyumbani kwako kama huna sensa utaishia maisha ya ajabu,” amesisitiza Zubeir.

Amesema Serikali inataka kujua ina watu wangapi ili ijue mahitaji yanayohitajika, “inataka kujua itatengeneza barabara kiasi gani mijini na vijijini, itajenga hospitali ngapi, shule ngapi, wanataka kuelewa, chakula kiasi gani, ajira, maji kiasi gani.

“Unataka sisi tufe kwa kupewa kidogo kumbe tuko wengi, vituo vya afya vichache kumbe tuko wengi, waalimu wangapi wanahitajika msingi hadi chuo kikuu, sensa hiyo.”

Sheikh Zubeir amesema anasimama sana kwenye suala hilo la sensa kutokana na miaka ya huko nyuma baadhi ya masheikh kupinga zoezi hilo.

“Nasimama sana katika suala la sensa kwasababu zamani kipindi cha Rais Jakaya Kikwete Masheikh walipinga na mimi nikasimama nikasema hapana, sensa ni jambo zuri,” amesema.

“Niwahimize Masheik wa mikoa wilaya, kata maimamu wawahimize waislamu kwenda kuhesabiwa na kuacha shughuli zao wakahesabiwe,” amesema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wauguzi, madaktari 1000 kugawiwa mitungi ya Oryx Gas

Spread the loveKAMPUNI ya Oryx Gas na Taasisi ya Doris Mollel Foundation...

Habari Mchanganyiko

Tanzania yachaguliwa Makamu wa Rais Tume ya Shirika la Hali ya Hewa Duniani

Spread the love  TANZANIA kupitia Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA)...

Habari Mchanganyiko

NEMC yaonya wanaojenga bila tathmini ya mazingira

Spread the loveBARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC),...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB Pesa Akaunti yawavutia wakaguzi wa ndani Afrika

Spread the loveUbunifu wa bidhaa bora wa Benki ya NMB pamoja na...

error: Content is protected !!