Tuesday , 23 April 2024
Home Habari Mchanganyiko ATCL yarejesha safari za Dar es Salaam-Guangzhou
Habari MchanganyikoTangulizi

ATCL yarejesha safari za Dar es Salaam-Guangzhou

Spread the love

SHIRIKA la Ndege Tanzania (ATCL) imerejesha safari za kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou China kuanzia tarehe 17 Julai, 2022. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

ATCL imetoa taarifa kwa umma kuuharifu kuhusu kurejea kwa safari hizo zitakazokuwa zikifanyika siku za Jumapili saa 11.15 asubuhi na kurejea siku za Jamatatu saa 1.15 asubuhi.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana tarehe 9 Julai, 2022, imeeleza kuwa nauli ya dajara la kawaida itakuwa ni Dola za Marekani 4,800 na dola za Marekani 6,850 kwa daraja la biashara.

“Nauli hii ni kwa safari moja kutoka Dar es Salaam kwenda Guangzhou-China na zimejumuisha gharama zote za usafiri,” imeeleza taarifa hiyo.

Taaria hiyo imeeleza zaidi kuwa tiketi zote zitauzwa katika ofisi za ATCL makao makuu, “ATCL haitahusika na tiketi itakayokuwa imenunuliwa kwa bei tofauti itakayouzwa nje ya ofisi yetu ya mauzo. Hata hivyo, kwa safari za kuanzia Guangzhou- China kuja Dar es Salaam, tiketi zitauzwa katika ofisi zetu zote za mawakala wetu wote. Msafiri anatakiwa kuwa na vibali vyote husika pamoja na VISA kabla ya safari yake.”

Kampuni hiyo imesema inapitia upya takwa la karantini ya siku tano na gharama zake kwa wasafiri waendao Guangzhou- China ili kuhakikisha kuwa hakuna msafiri mwenye maambukizi ya UVIKO-19 ambaye atasafiri na ATCL.

Aidha litapitia muda wa karantini wa wasafiri wake ili kuhakikisha zinaendana na utaratibu unaotumika nchini China na pia itapiotia gharama za mahoteli yaliyopendekezwa na wawakilishi  wa Jumuiya wa Wachina ili kuhakikisha inakuwa nafuu kwa wasafiri.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

NMB yadhamini Mkutano Mkuu ALAT, kufunguliwa na Samia

Spread the loveBENKI ya NMB, imekabidhi hundi yenye thamani ya Sh. 120...

Habari Mchanganyiko

DC ampongeza Dk. Rose Rwakatare kwa kusaidia waathirika wa mafuriko Mlimba

Spread the loveMWENYEKITI wa Wazazi CCM Mkoa wa Morogoro, Dk.  Rose Rwakatare...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mipango na uwekezaji kutumia bilioni 121.3, mradi wa Bagamoyo wapewa kipaumbele

Spread the loveWIZARA ya Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, imeliomba Bunge...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Mbunge ataka kasi uzalishaji walimu ipunguzwe akidai hakuna ajira

Spread the loveMBUNGE wa Mlalo (CCM), Rashid Shangazi, ameishauri Serikali ipunguze kasi...

error: Content is protected !!