Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa JUKATA waanika sababu Dk. Ndumbaro kung’olewa
Habari za SiasaTangulizi

JUKATA waanika sababu Dk. Ndumbaro kung’olewa

Dk. Damas Ndumbaro
Spread the love

JUKWAA la Katiba Tanzania (Jukata) limeeleza kuwa mojawapo ya sababu ya kuhamishwa Dk. Damas Ndumbaro kutoka Wizara ya Katiba na Sheria kuelekea wizara ya sanaaa, utamaduni na michezo, ni kutozingatia maelekezo ya Rais Samia Suluhu Hassan namna ya kutekeleza mchakato wa Katiba mpya. Anaripoti Faki Sosi …(endelea).

Hayo yameelezwa na Mjumbe wa Jukwaa hilo Deus Kibamba wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo tarehe 31 Agosti 2023.

Ananilea Nkya

Kibamba amesema Dk. Ndumbaro alikwenda kinyume na maagizo ya Rais ambaye aliagiza kuanzishwa kwa mchakato wa Katiba mpya haraka lakini yeye aliutangazia umma kuwa serikali itatoa elimu kwa wananchi kwa muda wa miaka mitatu.

“Alikuwa anauambia umma kuwa serikali itatoa elimu juu ya Katiba 1977… aliturudisha miaka 12 nyuma kwa sababu katiba hii ilikuwa inaelimishwa  wakati wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba maarufu kama Tume ya Jaji Warioba ambayo ilikusanya maoni ya wananchi kuhusu Katiba hiyo, hivyo tusingetegemea mtu aturejeshe kwenye mchakato huo wa elimu tena,” amesema Kibamba.

Amesema haamini kauli iliyotolewa na Dk. Ndumbaro ni msimamo wa Serikali ndio maana amechaguliwa Waziri Pindi Chana atakayeongoza mchakato huo.

Mkurugenzi wa Jukata, Bob Chacha Wangwe

“Tunaamini huyu Balozi Pindi Chana, Rais ameshauriwa na vyombo vyake kuwa huyu ndiye atajayeweza kuupeleka mbele mchakato huo,” amesema.

Aidha, Mkurugenzi wa Jukata, Bob Chacha Wangwe amesema jukwaa hilo limefanya mchakato wa kuandaa sheria ya mfano itakayoiongoza serikali kwa ajili ya Katiba mpya.

Bob amesema kuwa sheria hiyo ni zao la maoni ya wananchi, wanasiasa, wanahabari, wanazuoni, viongozi wa dini, asasi za kiraia, Kamati ya Bunge ya Katiba na sheria, Tume za marekebisho ya sheria kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.

Amesema jukwaa hilo limependekeza serikali kuachana na mpango wa utoaji elimu ya katiba ya mwaka 1977 kwa miaka mitatu kama ilivyoelezwa na Dk. Ndumbaro badala yake kuendelea na mchakato huo kama ilivyopendekezwa na Kikosi Kazi kilichoundwa na Rais Samia.

Bob ametoa wito kwa waziri wa sasa wa Katiba na Sheria, Balozi Chana kutoa ratiba ya hatua za mchakato wa Katiba Mpya.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!