RAIS Samia Suluhu Hassan ametembelea ujenzi wa Kituo cha Afya cha Kizimkazi kilichopo Mkoa wa Kusini Unguja kinachojengwa na Serikali kwa kushirikiana na Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) ikiwa ni jitihada za wadau hao wawili katika kuimarisha huduma za afya kwa wananchi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).
Ziara ya Rais Samia kwenye eneo hilo la mradi imefanyika leo Alhamisi ikiwa pia ni sehemu ya ufungaji wa Tamasha la Kizimkazi 2023.

Katika ziara hiyo Rais Samia aliambatana na viongozi waandamizi kutoka serikalini na Chama tawala cha CCM akiwemo Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo, Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Rashid Hadidi, viongozi waandamizi wa benki ya NBC wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi pamoja na wakazi wa eneo hilo.

Akizungumzia mradi huo wenye thamani ya Sh 4.4 bilioni ambapo benki ya NBC imechangia kiasi cha Sh 400 milioni, Rais Samia pamoja na kuipongeza NBC kwa hatua hiyo muhimu.

Amesema ni lengo la serikali kuboresha huduma ya afya kwa kujenga vituo vya afya kwenye maeneo mbalimbali kulingana na uhitaji mkubwa wa huduma hiyo katika maeneo hayo.
Leave a comment