Tuesday , 26 September 2023
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yawapa kibarua mawaziri wapya
Habari za SiasaTangulizi

CCM yawapa kibarua mawaziri wapya

Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara
Spread the love

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka mawaziri na manaibu mawaziri walioteuliwa hivi karibuni na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, kuyafanyia tathmini  maeneo ya ilani ya uchaguzi ya chama hicho ya 2020, ambayo hayajatekelezwa ili  yafanyiwe kazi kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025. Anaripoti Mwandishi Wetu, Zanzibar…(endelea).

Agizo hilo limetolewa leo tarehe 1 Septemba 2023 na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Abdulrahman Kinana, katika hafla ya uapisho wa mawaziri hao, iliyofanyika visiswani Zanzibar.

“Sasa tuko nusu ya muhula wa miaka mitano tangu tulipochaguliwa 2020, 2025 kutakuwa na uchaguzi na tumeahidi watanzania kupitia ilani ya uchaguzi. Sasa ni wakati muafaka kwa kila mmoja wenu kutathimini utekelezaji wa ilani ambayo ndiyo mkataba kati ya watanzania, CCM na Serikali yao,” amesema Kinana na kuongeza:

“Rais amewaamini, watanzania wana matumaini na ninyi, kila mmoja wenu atumie fursa hii kuona nusu ya muhula huu tumefanikiwa kwa kiasi gani, tumebakia kiasi gani na tunatakiwa kuongeza kasi kwa namna gani. Kama Rais alivyo na matumaini kwenu na mimi na watanzania tuna matumaini sana na nyie.”

Miongoni mwa mawaziri walioteuliwa au kuhamishwa wizara ni Dotto Biteko, aliyeteuliwa kuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati. Mbunge wa Ukonga, Jerry Silaa, aliyeteuliwa kuwa Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi. January Makamba, aliyehamishiwa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, akitokea Wizara ya Nishati.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia avunja bodi ya REA

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua Balozi Jacob Kingu, kuwa...

Habari za SiasaTangulizi

Chande aliyeng’olewa TANESCO kwenda TTCL apelekwa Posta

Spread the loveRAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amemteua aliyekuwa, Mkurugenzi Mkuu wa...

Habari za Siasa

Kamugisha aanika utekelezaji mpango kazi 2022/23

Spread the loveMWENYEKITI wa Ngome ya Vijana ya Chama Cha ACT-Wazalendo Mkoa...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo wakabidhiwa kivumbi kulinda kura uchaguzi 2024,2025

Spread the loveNGOME ya Vijana ya Chama cha  ACT-Wazalendo, imetakiwa kuwanoa wafuasi...

error: Content is protected !!