Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Habari Kimataifa Mwanaye rais aliyepinduliwa Gabon, afumwa na mabegi ya pesa
KimataifaTangulizi

Mwanaye rais aliyepinduliwa Gabon, afumwa na mabegi ya pesa

Spread the love

Mabegi, mifuko pamoja na masanduku yaliyojazwa fedha za nchi mbalimbali yamekutwa ndani ya nyumba ya Yann Ngulu mtoto mkubwa wa Rais Ali Bongo aliyeondolewa madarakani na Jeshi mapema wiki hii. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa …(endelea).

Hayo yamejiri siku chache baada ya Rais Ali Bongo, kuondolewa madarakani kisha Jeshi la nchi hiyo kuanza kufanya msako na upekuzi katika mali zake.

Imedaiwa kuwa mapema usiku wa kuamkia leo tarehe 31 Agosti 2023, katika nyumba ya mtoto mkubwa Yann Ngulu walikuta Mabegi, mifuko na masanduku yakiwa yamejazwa fedha.

Hata hivyo, kiasi cha pesa taslim hakijulikani kwani mifuko hiyo ilijazwa pesa za nchi tofauti tofauti za sarafu ya Dola za Marekani, Euro, na Franc.

Vyombo vya habari vya nchi hiyo vimeripoti kuwa, hatua hiyo imeibua hasira kwa raia wa nchi hiyo hasa ikizingatiwa kiongozi huyo anatuhumiwa kwa rushwa, ukosefu wa usawa wa kiuchumi na matumizi mabaya ya madaraka.

Mapema leo, Jeshi la Gabon lililompindua Rais Bongo limemteua Jenerali Brice Oligui Nguema kuwa kiongozi mpya wa nchi hiyo.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Sabaya afutiwa kesi, ruksa kugombea uongozi

Spread the loveMwendesha Mashtaka Mkuu wa Serikali DPP leo Ijumaa amefuta rufaa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kwafukuta kisa chaguzi, Lissu aibua tuhuma nzito

Spread the loveCHAGUZI za kusaka viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo...

Habari MchanganyikoTangulizi

Kimbunga “HIDAYA” chaendelea kuimarika, wananchi wapewa tahadhari

Spread the loveMAMLAKA ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) inaendelea kutoa taarifa...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema kumshtaki Rais Samia

Spread the loveCHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimetishia kumfungulia kesi ya...

error: Content is protected !!