MKUU wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Meja Jenerali Charles Mbuge, amewarejesha katika mafunzo, vijana waliochaguliwa kujiunga na JKT kwa kujitolea kwa mwaka 2020/2021. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).
Ni baada ya kurejeshwa nyumbani Februari 2021.
Akitoa taarifa hiyo leo Ijumaa, tarehe 30 Aprili 2021, jijini Dodoma, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Hassan Mabena amesema, vijana hao wanatakiwa kuripoti katika kambi walizokuwa wamepangiwa awali kuanzia tarehe 7-14 Mei 2021.
Amesema, vijana waliorejeshwa ni wale wenye elimu ya darasa la saba na kidato cha nne.
“Vijana wenye elimu ya kidato cha sita, ngazi ya cheti, stashahada, shahada na wale wenye taaluma ya uhandisi wataendelea kusubiri majumbani hadi hapo utaratibu mwingine utakapotangazwa,” amesema
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) limekuwa likiendesha mafunzo yakuwajengea uwezo vijana kwa kuwapa stadi za maisha ikiwa ni pamoja na uzalishaji mali, uzalendo, kilimo, ufugaji na kushiriki katika ujenzi wa Taifa.
Leave a comment