
KLABU ya Simba imepangwa kucheza na Kaizer Chiefs kwenye hatua ya robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchezeshwa kwa droo. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).
Droo hiyo imechezeshwa leo tarehe 30 Aprili, 2021 jijini Cairo, nchini Misri kwenye makao makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Simba imefuzu kwenye hatua hiyo baada ya kuibuka vinara kwenye kundi A, wakiwa na pointi 13, huku Kaizer Chief wakishika nafasi ya pili kwenye kundi C wakiwa na pointi tisa.

Kwenye mchezo wa kwanza Simba itaanzia ugenini nchini Afrika Kusini tarehe 14 Mei, 2021 na mchezo wa marudiano utachezwa tarehe 21-22 Mei 2021, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.
Michezo mingine kwenye hatua hiyo itaikutanisha Al Ahly dhidi ya Mamelod Sundown, Wydad Casablanca dhidi ya MC Alger na CR Belouizdad itamenyana na Esparance de Tunis.
Kama Simba itafanikiwa kupita kwenye hatua hiyo itakutana na mshindi wa kwenye mchezo kati ya Wydada Casablanca dhidi ya MC Alger.
More Stories
Prof. Asad: Katiba mpya muhimu, nchi imefunguka
Mauya miwili tena Yanga
Nabi: ubingwa bado, subirini kidogo