May 26, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Orlando vs Raja Casablanca, Robo fainali Shirikisho CAF

Spread the love

 

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepanga droo ya hatua ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho ambapo Orlando Pirates kutoka Afrika Kusini itamenyana na Raja Casablanca kutoka Morocco, huku Enyimba ya Nigeria itaanzia ugenini dhidi ya Pyramids kutoka Misri. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Droo hiyo imechezeshwa Makao Makuu ya shirikisho hilo jijini Cairo, nchini Misri majira ya saa 9 jioni.

Michezo mingine itakuwa kati ya Coton Sport kutoka nchini Cameroon ambao watakuwa nyumbani dhidi ya ASC Jaraaf kutoka nchini Senegal.

Kwa upande wa CS Sfaxien kutoka nchini Tunisia wao watakuwa nyumbani kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya JS Kabylie ya nchini Tunisia.

Michezo hiyo ya nusu fainali itaanza kuchezwa kuanzia tarehe 23 Mei 2021, na nusu fainali ya kwanza itapigwa tarehe 27 Juni, 2021

error: Content is protected !!