WAHITIMU wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki (HKMU), watakiwa kutumia elimu waliyoipata kufanya tafiti na kutatua changamoto mbalimbali zilizoko kwenye jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea)
Hayo yamesemwa leo chuoni hapo na aliyekuwa Naibu Waziri wa Fedha, janeth Mbele, wakati wa mjadala kuhusu masuala ya biashara na uchumi kuelekea mahafali ya 21 yanayofanyika kesho Jumamosi chuoni hapo.
Alisema wanapomaliza Shahada au Stashahada kwenye udaktari uuguzi au ustawi wa jamii wasione wamefika mwisho na badala yake waendelee kutauta fursa zikiwemo za ujasiriamali.
Alisema vyuo vinatoa wahitimu wengi lakini soko la ajira ni dogo hivyo wanapaswa kuwa wabunifu kwa kutafuta mbinu za kujiajiri wenyewe na kuajiri wenzao kwa kutumia ujuzi walionao.
Alisema pamoja na changamoto za huduma za kiafya zinapaswa kuwa fursa kwa na kwenye changamoto nyingi ndiko kwenye fursa hivyo waaanzishe huduma za afya na kuanzisha biashara za huduma hizo.
“Wahitimu wawe wabunifu watoe suluhisho kwa changamoto hizo kwa kuanzisha shughuli mbalimbali ambazo zitaleta suluhisho na tatizo haliwezi kuwa mtaji kama wengine ambao wamekuwa wakitoa visingizo,” alisema
Aliwataka pia kujiendeleza kiteknolojia kwa kuanzisha huduma za kisasa ambazo mara nyingi huwa hazipatikani hasa maeneo ya vijijini hususan kwenye huduma za afya.
“Kama ni daktari, muuguzi unaweza kutumia ujuzi wako kwa kutumia teknolojia kuwahudumia wananchi walioko pale na uwe tayari kujituma kwasababu huduma hizi ni za wito isiwe tu ni ajira uwe na shauku ya kuwahudumia wananchi,” alisema
“Ndiyo maana wakati mwingine daktari au muuguzi anaitwa saa nane usiku anakwenda kuwahudumia wagonjwa kwasababu ana wito na kazi yake,” alisema
Mbene alikipongeza chuo cha HKMU kwa kuanzisha program atamizi kuwasaidia wahitimu kuanzisha na kuendeleza biashara zao badala ya kutegemea fani zao pekee.
Alisema wahitimu wanapaswa kutumia fursa zilizopo na washirikiane na wenzao kufanya jambo kwa pamoja kwani kwa kufanya hivyo wanaweza kuona matokeo mazuri mapema kuliko kila mtu kuwa kivyake vyake.
“Nimewapa changamoto wkenye amsuala ya ubunifu kwasababu kwenye mataifa mengi yaliyoendelea wahitimu wao wanakwenda kubuni vitu sasa na watanzania nao wafanye waache visingizo kwamba fursa ni chache watumie mazingira yaliyopo kutengeneza fursa,” alisema
Kuhusu mikopo ya elimu ya juu, Mbene aliitaka serikali kuwa makini na kuhakikisha wanaopewa mikopo hiyo ni wale wanaostahili kwani kumekuwa na malalamiko kwamba watu sahihi wanakosa na wanapewa watu wasiostahili.
“Haya malalamiko mmeyasikia kwa hiyo mimi ninachoweza kusema ni kwamba serikali iwe makini ili wanaopata wawe kweli wale wanaostahili kupata kwasabbau wakipata wenye uwezo inakuwa haina maana,” alisema
Leave a comment