Friday , 1 March 2024
Home Kitengo Maisha Afya GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi
AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the love

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko amewataka wadau mbalimbali wanaohusika na mapambano dhidi ya UKIMWI nchini kwa kushirikiana na Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kuhakikisha kuwa wanatenga fedha za kutosha kwa ajili ya mapambano dhidi ya UKIMWI nchini badala ya kutegemea wafadhili kwa kiasi kikubwa. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Dk. Biteko amesema hayo jana katika mkutano maalum wa wadau wanaoshughulikia udhibiti wa UKIMWI Tanzania uliofanyika mjini Morogoro na kuhusisha viongozi wa Serikali, wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wadau wa maendeleo ikiwamo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML).

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko (katika) akiwa na viongozi mbalimbali wa serikali pamoja na wadau wa maendeleo ikiwamo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ambayo iliwakilishwa na Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dk. Kiva Mvungi (wa kwanza kulia waliosimama) na Meneja Uhusiano na Mawasiliano, Stephen Mhando (wa kwanza kushoto waliosimama).

Alisema pamoja na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali pamoja na wadau, bado UKIMWI haujadhibitiwa inavyotakiwa, hali inayoweza kusababisha maambukizi mapya kuongezeka.

Aliwataka wadau wote wanaohusika kuendelea na juhudi za utoaji afua mbalimbali zenye lengo la kutokomeza ugonjwa wa UKIMWI.

“Tanzania imepiga hatua kubwa katika mapambano dhidi ya UKIMWI na nawataka TACAIDS na wadau kuhakikisha mnashirikiana kwa pamoja dhidi ya mapambano ya Ukimwi kwa kuongeza ushiriki wa wananchi pia,” amesisitiza Dk. Biteko.

Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko (katika) akihutubia na viongozi mbalimbali wa serikali, wanaoishi na virusi vya UKIMWI na wadau wa maendeleo ikiwamo Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) katika mkutano maalum wa wadau wanaoshughulikia udhibiti wa UKIMWI Tanzania uliofanyika juzi mjini Morogoro.

Aidha, akichangia mada katika mkutano huo, Meneja Mwandamizi wa Afya, Usalama, Mazingira na Mafunzo wa GGML, Dk Kiva Mvungi aliunga mkono hoja hizo za Dk. Biteko na kusisitiza kuwa maeneo mengine ambayo Serikali inaweza kutumia na kupunguza utegemezi wa wafadhili ni kupitia kampuni kubwa zinazofanya shughuli zake hapa nchini.

“Kwa mfano GGML hushirikiana na TACAIDS kila mwaka kuandaa kampeni ya Kili Challenge ambayo  washiriki hupanda na kuuzunguka mlima Kilimanjaro na fedha zinazopatikana huelekezwa katika mfuko wa kudhibiti Ukimwi pamoja na kuwezesha afua na asasi zinazojishughulisha na masuala ya Ukimwi,” alisema.

Dk. Kiva alitaja mbinu nyingine ya kuondokana na utegemezi kutoka kwa wafadhili kuwa ni kushirikisha Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) ambacho kina wanachama mbalimbali wakiwamo makampuni makubwa ya madini na kampuni nyingine ambazo zitaweza kuchangia fedha za kuendeleza mapambano dhidi ya VVU/ Ukimwi.

“Kwa kutumia ATE tunaweza kushirikisha wafanyakazi wetu au kuwatia moyo wanachama  wa ATE wawe na mtazamo na kusaidia jamii na kufanya tathmini ya mahali ambapo mtu au kampuni husika inapofanya kazi. Kisha tunaingia kwenye jamii za kupima kama kweli huduma hizo muhimu za elimu ya afya zimetolewa.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Jerome Kamwela alisema mkutano huo unalenga kutoa nafasi ya mashaurinao kati ya Serikali na wadau wake katika mapambano dhini ya UKIMWI.

Alisema mkutano  huo ni muhimu hasa wakati huu ambao Tanzania inaelekea kufikia lengo la dunia la kumaliza UKIMWI ifikapo mwaka 2030.

“Lengo linataka kusiwe na maambukizi mapya ya UKIMWI, kusiwe na vifo vinavyotokana na UKIMWI pia, kusiwe na unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi,” alisema.

1 Comment

  • Je, hizo kampuni kubwa si za wawekezaji wa nje?
    Vizazi vipya vya X (Millennium) na Z vinadhani UKIMWI ni wa vizazi vilivyopita.
    Sasa kama UKIMWI unaongezeka kwa kasi, kwa nini elimu haitolewi sekondari na vyuoni.
    Atakayempa mwenzie UKIMWI apelekwe jela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Karafuu, Parachichi yawa fursa Morogoro

Spread the loveIMEELEZWA kuwa zao la karafuu ambalo kwa sasa linalimwa pia...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Washindi 12 NMB MastaBata na wenza wao wapaa Afrika Kusini

Spread the loveWASHINDI 12 wa kampeni ya kuhamasisha matumizi yasiyohusisha pesa taslimu...

Habari Mchanganyiko

4 wanusurika kifo ajali ya ndege Serengeti

Spread the loveWATU wanne wakiwamo abiria watatu na rubani mmoja wamenusurika kifo...

AfyaTangulizi

Kitita cha NHIF kuanza Ijumaa, kuwapa wanachama nafuu zaidi

Spread the love  MFUKO wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umetangaza...

error: Content is protected !!