JESHI la Israel limesema kuwa limeshambulia maeneo yenye uhusiano na kundi la wapiganaji wa Palestina Hamas ndani ya Lebanon na katika Ukanda wa Gaza. BBC imeripoti … (endelea).
Mashambulizi hayo yanakuja baada ya shambulio kubwa la roketi dhidi ya Israel kutoka Lebanon, ambalo Waisraeli walilaumu kundi la Hamas.
Jeshi la Ulinzi la Israel lilisema miundombinu ya “kigaidi” ya Hamas ilipigwa kusini mwa Lebanon.
Hali ya wasiwasi imetanda baada ya polisi wa Israel kuvamia msikiti wa Al-Aqsa mjini Jerusalem usiku mtawalia mapema wiki hii.
Msikiti huo ni eneo la tatu takatifu kwa Uislamu, na uvamizi wa Israel umezusha makabiliano makali na Wapalestina ndani na kusababisha hasira katika eneo hilo kubwa.
Mkuu wa Hamas Ismail Haniyeh, ambaye alikuwa Lebanon wakati roketi hizo ziliporushwa, alisema Wapalestina “hawataketi wakitazama tu” uvamizi wa Israel ukiendelea.
Katika taarifa mapema siku ya Ijumaa, IDF iliandika kwenye Twitter kwamba ilikuwa imejiwekea melenga ya mahali pa kushambilia “ikiwa ni pamoja na miundombinu ya kigaidi ya Hamas kusini mwa Lebanon”.
IDF iliongeza kuwa haitaruhusu Hamas kufanya kazi kutoka Lebanon na kushikilia Lebanon “kuwajibika kwa kila moto ulioelekezwa kutoka katika eneo lake”.
Leave a comment