Tuesday , 7 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Hima yajitosa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia
Habari Mchanganyiko

Hima yajitosa mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia

Mkurugenzi wa Hima Organization Tanzania, Francisca Mawalla
Spread the love

 

SHIRIKA la Hima Organization Tanzania, limeanza kutoa mafunzo kwa makundi mbalimbali, juu ya namna ya kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mafunzo hayo ya siku moja yamefanyika leo tarehe 19 Septemba 2023, maeneo ya Kunduchi Mtongani, mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza katika mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Hima Organization Tanzania, Francisca Mawalla,amesema wameanzisha ili kusaidia harakati za kupambana na rushwa ya ngono, ukatili wa kijinsia na kiuchumi.

“Tuko hapa kupambana na ukatili wa kijinsia, rushwa ya ngono na kutoa elimu ya kiuchumi na ujasiriamali, tumeanzisha shirika hili baada ya kuona uhitaji mkubwa wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia , hivyo tutawasaidia wahanga wakipata changamoto ili wajue wapi pa kuzipelekea na kupata majibu,” amesema Mawalla.

Diwani wa Kata ya Kunduchi, Michale Urio, alilitaka shirika hilo kutoa elimu kwa makundi yote hususan watoto ili waweze kuripoti wanaofanya vitendo vya ukatili wa kijinsia dhidi yao katika mamlaka husika.

“Mfano sasa hivi darasa la saba wamemaliza shule, hili ni jukumu lenu nawapa muandae kongamano mkawape elimu ya ukatili wa kijinsia ili watakapopangiwa shule katika maeneo mbalimbali wawe na uelewa juu ya suala hilo na kujua namna ya kujilindi,” amesema Urio.

Naye Afisa Maendeleo wa Kata ya Kunduchi,Theresia Kimario, amewataka wazazi na walezi kuwa karibu na watoto wao ili wapate kujua masuala yanayowasibu kwani baadhi yao hushindwa kuwasilisha vitendo vya ukatili wa kijinsia wanavyofanyiwa, kutokana na wao kukosa muda.

“Unakuta mtoto anakuja kwa mzazi anamuelezea shida zake, mzazi anamfukuza toka bila kumsikiliza. Wapo watoto wanapitia mazingira magumu tunapaswa kuwasikia ili tuwasaidie kabla hawajaharibika,” amesema Kimario.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Mahakama yatoa uamuzi zuio dhidi ya Club House

Spread the loveMAHAKAMA Kuu ya Tanzania, Masjala Kuu jijini Dar es Salaam,...

Habari Mchanganyiko

GGML, OSHA yawanoa bodaboda 200 Arusha

Spread the loveZAIDI ya madereva bodaboda 200 wa jiji la Arusha wamepatiwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Serikali kuwakopesha wajasiriamali 18.5bn/- kupitia NMB

Spread the loveSerikali imetenga kiasi cha Sh 18.5 bilioni kwa ajili ya...

AfyaHabari Mchanganyiko

Huduma za kibingwa zazinduliwa katika hospitali za halmashauri 184

Spread the loveSERIKALI imezindua huduma za matibabu za kibingwa katika hospitali 184...

error: Content is protected !!